Kuhusu kupiga akaunti marufuku


Ikiwa akaunti yako imepigwa marufuku, utaona ujumbe ufuatao unapofungua WhatsApp: "Akaunti hii hairuhusiwi kutumia WhatsApp."
Huwa tunapiga akaunti marufuku ikiwa tunaamini kuwa shughuli ya akaunti inakiuka Masharti yetu ya Huduma, kwa mfano, ikiwa inahusisha taka, ulaghai au ikiwa inahatarisha usalama wa watumiaji wa WhatsApp.
Kama unadhani akaunti yako ilipigwa marufuku kwa makosa, tafadhali tutumie barua pepe au gusa omba ukaguzi kwenye programu ili tuweze kuangalia suala lako. Tutawasiliana nawe mara tu tutakapokamilisha ukaguzi wetu.
Unapoomba ukaguzi katika programu, utaombwa uweke msimbo wa usajili wenye tarakimu 6 uliotumwa kwako kupitia SMS. Mara baada ya kuuweka, utaweza kuwasilisha ombi lako la ukaguzi na kuongeza maelezo ili kutetea suala lako.
Tunapendekeza ukague kwa makini sehemu ya “Matumizi Yanayokubalika ya Huduma Zetu” katika Masharti yetu ya Huduma ili uelewe zaidi kuhusu matumizi sahihi ya WhatsApp na shughuli zinazokiuka Masharti yetu ya Huduma.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La