Jinsi ya kuchagua mahali unapotafuta biashara

Kumbuka: Kipengele hiki huenda bado hakipatikani mahali ulipo.
Una machaguo mawili unapotafuta biashara:
  • Shiriki mahali ulipo sasa. Data ya mahali huhifadhiwa kwenye simu yako na itapakiwa upya tu ikiwa utashiriki mahali ulipo tena. WhatsApp wala biashara kwenye saraka, haziwezi kuona mahali ulipo. Matokeo ya biashara hupangwa kulingana na umbali na ishara nyinginezo na unaweza kufuta data yako ya mahali iliyohifadhiwa kutoka kwenye simu yako wakati wowote.
  • Chagua mahali. Hatua hii ni muhimu kwa watu ambao hawataki kushiriki maelezo ya mahali vifaa vyao vilipo au kwa watu wanaotafuta biashara zilizo karibu na mahali wanapofanyia kazi au mahali ambapo rafiki anaweza kuwa anaishi.
Kuhusu faragha ya mahali
Kabla ya WhatsApp kutumia data ya mahali ulipo ili kukusaidia kupata biashara zilizo karibu, taarifa zako za mahali hubadilishwa kuwa mahali pasipo sahihi ili WhatsApp isijue ni wapi hasa ulipo. Matokeo ya utafutaji mpana hurejeshwa kwenye simu yako na kuorodheshwa kulingana na umbali hadi eneo halisi, pamoja na ishara nyinginezo. Kwa njia hii, seva za WhatsApp kamwe hazioni mahali mahususi ulipo.
Tafadhali kumbuka kuwa WhatsApp hutumia Google kama mtoa huduma kutoka shirika lingine na kwa hivyo data ya mahali itashirikiwa na Google.
Kumbuka: Unapoanzisha soga na biashara uliyoipata kupitia tafuta biashara, biashara itapokea arifa kutoka WhatsApp ikiiambia kuwa uliipata kwa kutumia tafuta biashara. Mahali ulipo hubaki faragha na hapaonekani kwa biashara au WhatsApp.
Badilisha maelezo ya mahali ulipo
WhatsApp itatumia kwa chaguomsingi maelezo ya mahali uliyochagua ulipotafuta biashara mara ya mwisho. Unaweza kufuta maelezo hayo ya mahali na kuweka mapya.
  1. Kutoka kwenye skrini ya kutafuta ya biashara, gusa mahali.
  2. Gusa Orodha ya Majina na Mahali > Futa eneo lililowekwa sasa > FUTA.
  3. WhatsApp itatumia namba yako ya simu ili kubaini mahali ulipo kwa ujumla.
Kuacha kushiriki mahali ulipo
Wewe ndiwe unayedhibiti ikiwa ungependa kushiriki mahali pako na unaweza kuacha kushiriki mahali pako wakati wowote.
Kuacha kushiriki mahali ulipo kwenye WhatsApp
  1. Fungua Mipangilio kwenye kifaa chako.
  2. Gusa Mahali > Uwezo wa programu kufikia mahali > WhatsApp.
  3. Chagua Kataa.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La