Jinsi ya kusasisha WhatsApp

Unaweza kusasisha WhatsApp kwa urahisi kutoka kwenye duka la programu la simu yako. Tafadhali kumbuka, kama ulipokea ujumbe kwamba toleo lako la WhatsApp haliwezi kutumika tena, utahitaji kusasisha programu.
Tunakuhimiza utumie toleo jipya la WhatsApp kila wakati. Matoleo mapya yana vipengele vipya zaidi na marekebisho ya hitilafu.
Android
Tafuta WhatsApp Messenger kwenye Duka la Google Play, kisha uguse Sasisha.
iPhone
Tafuta WhatsApp Messenger kwenye Duka la Programu la Apple, kisha uguse SASISHA.
KaiOS
Bonyeza JioStore au Hifadhi kwenye menyu ya programu. Sogeza kuelekea upande ili uchague Jamii, kisha uchague WhatsApp. Bonyeza SAWA au CHAGUA > SASISHA.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La