Jinsi ya kuongeza anwani

Android
KaiOS
iPhone
Unaweza kuongeza waasiliani kupitia WhatsApp au kitabu cha anwani cha simu yako.
Kuongeza mwasiliani kwa kupitia WhatsApp
  1. Bonyeza Soga mpya > Hiari > Ongeza mwasiliani mpya.
    • Kwenye JioPhone au JioPhone 2, utahitaji kuchagua kama unataka kuhifadhi mwasiliani kwenye Kumbukumbu ya simu au Kumbukumbu ya SIM.
  2. Ingiza jina la mwasiliani na namba ya simu > bonyeza HIFADHI.
  3. Mwasiliani ataingia moja kwa moja kwenye orodha ya waasiliani wako. Ikiwa mwasiliani haonekani, bonyeza Soga mpya > Hiari > Rejesha waasiliani.
Kuongeza mwasiliani kupitia kitabu cha anwani cha simu yako
  1. Bonyeza Waasiliani kwenye menyu ya programu.
  2. Bonyeza Mwasiliani mpya au Mpya.
    • Kwenye JioPhone au JioPhone 2, utahitaji kuchagua kama unataka kuhifadhi mwasiliani kwenye Kumbukumbu ya simu au Kumbukumbu ya SIM.
  3. Ingiza jina la mwasiliani na namba ya simu > bonyeza HIFADHI.
  4. Mwasiliani ataingia moja kwa moja kwenye orodha ya waasiliani wako wa WhatsApp. Ikiwa mwasiliani haonekani, fungua WhatsApp, kisha bonyeza Soga mpya > Hiari > Rejesha waasiliani.
Dondoo: Unaweza kumfuta mwasiliani kutoka kwenye kitabu cha anwani cha simu yako, lakini huwezi kumfuta kutoka WhatsApp.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La