Â
Jinsi ya kuongeza anwani
Android
KaiOS
iPhone
Kuna njia kadhaa za kuongeza anwani.
Kuongeza anwani kwenye soga mpya
- Nenda kwenye kichupo cha Soga.
- Gusa> Anwani mpya.
Kuongeza kutoka kwenye maelezo ya soga (namba ambazo hazijahifadhiwa ambazo umepiga nazo soga)
- Nenda kwenye kichupo cha Soga.
- Chagua soga kati yako na anwani ambayo haijahifadhiwa. Itawakilishwa na namba badala ya jina kwenye orodha ya soga.
- Gusa sehemu ya juu kwenye programu ili uone Maelezo ya Soga.
- Gusa Hifadhi kwenye chaguo zilizo juu ya skrini.
Kuongeza kutoka kwenye vikundi
- Gusa ujumbe kutoka kwa mtu asiye kwenye anwani zako > Ongeza kwenye Anwani.
- Chagua kwenye chaguo zifuatazo:
- Hifadhi: Hii itahifadhi anwani mpya.
- Ongeza kwenye Anwani Iliyopo: Andika jina la anwani iliyopo > gusa jina lililopo la anwani > Hifadhi.
- Ongeza kwenye Anwani Iliyopo: Andika jina la anwani iliyopo > Unda anwani mpya > Hifadhi.
Ili uongeze anwani inayotumia namba ya simu ya kimataifa, soma makala haya.