Jinsi ya kuhamisha data yako ya WhatsApp kutoka kwenye Android kwenda kwenye iPhone

Ikiwa unatoka kwenye simu ya Android hadi kwenye iPhone, unaweza kuhamisha taarifa za akaunti yako, picha ya jalada, soga binafsi, soga za vikundi, historia ya soga, maudhui na mipangilio. Huwezi kuhamisha historia yako ya simu zilizopigwa au jina la kuonyesha.
Ninahitaji nini?
 • Android OS Lollipop, SDK 21 au mpya zaidi au Android 5 au toleo jipya zaidi liwe limesakinishwa kwenye kifaa chako cha Android
 • iOS 15.5 au mpya zaidi iwe imesakinishwa kwenye iPhone yako
 • Programu ya Move to iOS iliyosakinishwa kwenye simu yako ya Android
 • Toleo la WhatsApp 2.22.10.70 au jipya zaidi kwenye kifaa chako kipya
 • Toleo la WhatsApp Android 2.22.7.74 au jipya zaidi kwenye kifaa chako cha zamani
 • Tumia namba ile ile ya simu kwenye simu yako ya zamani na katika kifaa chako kipya
 • iPhone yako lazima iwe mpya kama ilivyotoka kiwandani au weka upya mipangilio ya kiwandani ili kuoanisha na programu ya Move to iOS na kuhamisha data kutoka kwa simu yako ya Android
 • Vifaa vyako vyote viwili lazima viwe vimeunganishwa kwenye chanzo cha nishati
 • Vifaa vyako vyote viwili vinahitaji kuwa vimeunganishwa kwenye mtandao sawa wa Wi-Fi au utahitaji kuunganisha kifaa chako cha Android kwenye mtandao pepe wa iPhone yako
Kuhama Android kwenda kwenye iPhone
 1. Fungua programu ya Move to iOS kwenye simu yako ya Android kisha ufuate maelekezo yaliyo kwenye skrini.
 2. Msimbo utaonyeshwa kwenye iPhone yako. Unapoulizwa, weka msimbo huo kwenye simu yako ya Android.
 3. Gusa Endelea kisha ufuate vidokezo vilivyo kwenye skrini.
 4. Chagua WhatsApp kwenye skrini ya Hamisha Data.
 5. Gusa ANZA kwenye simu yako ya Android, halafu usubiri WhatsApp iandae data kwa ajili ya hamisha. Utaondolewa kwenye akaunti katika simu yako ya Android mara baada ya data kutayarishwa.
 6. Gusa INAYOFUATA ili urudi kwenye programu ya Move to iOS.
 7. Gusa ENDELEA ili kuhamisha data kutoka kwenye simu yako ya Android hadi katika iPhone yako na usubiri Move to iOS ithibitishe kuwa uhamishaji umekamilika.
 8. Sakinisha toleo la hivi karibuni la WhatsApp kutoka kwenye Duka la Programu.
 9. Fungua WhatsApp kisha uingie ukitumia namba ile ile ya simu uliyokuwa ukiitumia kwenye kifaa chako cha zamani.
 10. Gusa Anza utakapodokezewa kisha usubiri mchakato ukamilike.
 11. Maliza kuweka mipangilio kwenye kifaa chako kipya halafu utaona soga zako zikikungojea.
Kumbuka: Kwenda kwenye Faili na kuchagua folda ya WhatsApp katika programu ya Move to iOS hakutafanya kazi wakati wa uhamishaji.
Kitu gani kitafanyikia data yangu?
 • Data unayohamisha haiendi kwenye hifadhi ya wingu kutokana na uhamishaji unaoufanya mpaka utakapounda hifadhi rudufu ya iCloud.
 • WhatsApp haiwezi kuona data unayohamisha.
 • Simu yako ya Android bado itakuwa na data yako isipokuwa ukifuta WhatsApp au ukiondoa data yote kwenye simu yako.
Ni ujumbe gani ninaweza kuhamisha kwenda kwenye simu yangu mpya?
Unaweza kuhamisha:
 • Ujumbe wa binafsi
Huwezi kuhamisha:
 • Ujumbe wa malipo kati ya watu
Je, ninaweza kuhamisha historia yangu ya upigaji wa simu?
Historia yako ya simu zilizopigwa kwenye WhatsApp haiwezi kuhamishwa kutoka kwenye simu ya Android hadi kwenye iPhone.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La