Mhuri wa muda usio sahihi kwenye jumbe

Kama mhuri wa muda ulioonyeshwa kwenye jumbe ulizopokea au muda wa mwisho kaonwa ya waasiliani wako sio sahihi, tafadhali angalia saa na usanidi wa eneo la muda wa simu yako. Unaweza kuhitaji kuzirekebisha.
Tunapendekeza kuweka tarehe yako na saa iwe Otomatiki au Uliotolewa na Mtandao. Mpangilio huu ukiwezeshwa, mtoaji huduma wako wa simu ataweka simu yako kwa wakati sahihi. Ikiwa saa isiyo sahihi bado inaonyeshwa hata kama mpangilio huu umewezeshwa, basi kuna tatizo na mtandao wako. Tafadhali wasiliana na mtoaji huduma wako wa simu kusuluhisha.
Kusuluhisha, tafadhali badili mipangilio ya tarehe na saa na sahihisha eneo la muda mwenyewe.
Kumbuka: Eneo la muda ni tofauti na saa halisi. Hakikisha umechagua eneo la muda sahihi wa mahali pako.
Kusanidi eneo la muda mwenyewe, tafadhali fuata hatua hizi za simu yako:
  • Android: Nenda Mipangilio > Mfumo > Tarehe & Saa.
  • iPhone: Nenda Mipangilio > Jumla > Tarehe & Saa.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La