Jinsi ya kuomba maelezo ya akaunti yako
iPhone
Android
KaiOS
Kipengele cha kuomba maelezo ya akaunti kinakuruhusu kuomba na kuhamisha ripoti ya maelezo na mipangilio ya akaunti yako ya WhatsApp. Ripoti haitajumuisha ujumbe wako. Ikiwa unahitaji kufikia ujumbe wako kando ya kuwa kwenye programu, unaweza kuhamisha historia yako ya soga badala yake.
Kuomba ripoti
- Fungua WhatsApp.
- Bonyeza Chaguo > Mipangilio > Akaunti > Omba taarifa za akaunti.
- Chagua kisha ubonyeze Omba ripoti. Skrini itaonyesha arifa kuwa Ombi limetumwa.
Kwa kawaida ripoti yako itapatikana siku tatu baada ya tarehe unayotuma ombi. Unaweza kurejelea tarehe ya Itakuwa tayari mnamo unaposubiri ripoti yako.
Kumbuka:
- Mara tu unapoomba ripoti, huwezi kutengua au batilisha ombi lako linalosubiriwa.
- Ikiwa utabadilisha namba yako ya simu au kufuta akaunti yako, ombi lako unalosubiri litabatilishwa na utahitaji kuomba ripoti nyingine.
Kupakua na kuhamisha ripoti
Ripoti yako ikiwa tayari kupakuliwa, utapokea arifa ya WhatsApp kwenye simu yako, inayosema “Sasa ripoti ya taarifa za akaunti yako inapatikana”. Skrini ya Omba taarifa za akaunti kwenye WhatsApp itakuarifu kuwa utakuwa na wiki chache kupakua ripoti yako baada ya kupatikana, kabla haijafutwa kutoka kwenye seva. Kwa sababu ripoti hii ina maelezo yako, unapaswa uwe makini unapohifadhi, kutuma au kupakia kwa huduma zingine zozote.
- Fungua WhatsApp.
- Bonyeza Chaguo > Mipangilio > Akaunti > Omba taarifa za akaunti.
- Chagua kisha ubonyeze Pakua ripoti.
- Baada ya kupakua faili, bonyeza Hamisha ripoti > Sawa > Sawa.
Kumbuka: Baada ya kupakua ripoti kwenye simu yako, utakuwa na chaguo la kufuta kabisa nakala uliyoipakua kutoka kwenye simu yako kwa kuchagua na kubofya Futa ripoti > Sawa kwenye skrini ya Omba maelezo ya akaunti. Kufuta ripoti hakutafuta data yoyote ya akaunti yako ya WhatsApp.
Kuangalia ripoti
Hutaweza kuangalia ripoti uliyopakua kwenye WhatsApp. Kuangalia ripoti, utahitaji kuunganisha simu yako kwenye kompyuta.
- Kwenye kompyuta, tumia programu ya File Explorer kwenye Windows au pakua programu ya kuhamisha faili kama vile Android File Transfer kwenye Mac.
- Tumia waya ya USB ili kuunganisha simu yako kwenye kompyuta yako. Kwanza utahitaji kubonyeza Mipangilio kwenye menyu ya programu za simu yako > sogeza kando ili kuchagua Hifadhi > chagua kisha ubonyeze Hifadhi ya USB > chagua kisha ubonyeze Washa.
- Au, unaweza kuweka kadi ya SD ya simu yako kwenye kompyuta yako. Programu ya kutuma faili itafunguka kiotomatiki kwenye kompyuta.
- Kwenye kompyuta, bofya vipakuliwa > WhatsApp.
- Buruta faili ya My account info.zip hadi kwenye kompyuta.
- Ondoa zipu kwenye faili kwa kuifungua. Hii itaunda folda ya Maelezo ya akaunti yangu.
- Fungua folda hiyo, kisha ufungue faili ya HTML ili kuangalia maelezo ya akaunti yako.
Rasilimali zinazohusiana:
Jinsi ya kuomba maelezo ya akaunti yako