Jinsi ya kuomba taarifa za akaunti yako

iPhone
Android
KaiOS
Kipengele cha kuomba maelezo ya akaunti yako kinakuruhusu kuwasilisha ombi la ripoti na kuhamisha ripoti ya taarifa na mipangilio ya akaunti yako ya WhatsApp. Ripoti haitajumuisha ujumbe wako. Kama unahitaji kufikia ujumbe wako kando ya kwenye programu, unaweza kuhamisha historia yako ya soga badala yake.
Tafadhali kumbuka, kipengele hiki hakipatikani kwenye WhatsApp Web na Desktop.
Kuomba ripoti
  1. Nenda kwenye WhatsApp Mipangilio > Akaunti > Omba taarifa za akaunti.
  2. Gusa Omba ripoti. Skrini itajisasisha na kuonyesha Ombi limetumwa.
Kimsingi ripoti yako itapatikana siku tatu baada ya tarehe ulipoiomba. Unaweza kurejea tarehe ya Itakuwa tayari unaposubiri ripoti yako.
Kumbuka:
  • Mara tu unapoomba ripoti, huwezi kutengua au batilisha ombi lako linalosubiriwa.
  • Ukibadilisha namba yako ya simu au kufuta akaunti yako, ombi lako linalosubiriwa litabatilishwa na utahitaji kuomba ripoti nyingine.
Kupakua na kuhamisha ripoti
Wakati ripoti itakapokuwa tayari kupakuliwa, utapokea arifa ya WhatsApp kwenye simu yako, ikisema “Ombi lako la arifa za akaunti sasa linapatikana”. Skrini ya Omba taarifa za akaunti kwenye WhatsApp itakuambia idadi ya muda ulionao kupakua ripoti kabla haijafutwa kutoka kwenye seva zetu. Kwa kuwa ripoti hii ina taarifa zako, kuwa makini kuhusu kuhifadhi, kutuma au kuipakia kwenye huduma zingine.
  1. Nenda kwenye WhatsApp Mipangilio > Akaunti > Omba taarifa za akaunti.
  2. Gusa Pakua ripoti. Faili la ZIP litapakuliwa kwenye simu yako, pamoja na faili za HTML na JSOL.
  3. Baada ya faili kupakuliwa, gusa Hamisha ripoti > HAMISHA au Hamisha ripoti. Hutaweza kutazama ripoti uliopakua ndani ya WhatsApp.
  4. Kwenye machaguo ya kushiriki yanayotokea, gusa programu ya nje unayotaka kutumia kuhamisha ripoti yako. Kwa mfano, unaweza kujitumia nakala ya ripoti kwa barua pepe.
Baada ya kupakua ripoti kwenye simu yako, utakuwa na chaguo la kufuta moja kwa moja nakala ulilopakua kutoka kwenye simu yako kwa kugusa Futa ripoti > FUTA au Futa ripoti kwenye skrini ya Omba taarifa ya akaunti. Kufuta ripoti hakutafuta data yoyote ya akaunti yako ya WhatsApp.
Rasilimali zinazohusiana:
  • Jinsi ya kuomba taarifa ya akaunti yako kwenye KaiOS
  • Jinsi ya kuhamisha historia yako ya soga kwenye: Android | iPhone
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La