Ikiwa anwani hazionekani

iPhone
Android
Kwa hali bora ya utumiaji, tunapendekeza uruhusu WhatsApp ifikie anwani zako.
Kuruhusu ufikiaji wa anwani zako
 1. Nenda kwenye Mipangilio
  ya iPhone > Faragha na Usalama.
 2. Gusa Anwani.
 3. Hakikisha kuwa umewasha WhatsApp.
Ikiwa WhatsApp haipatikani, hakikisha kuwa huna vizuizi vyovyote ulivyoweka kwenye
Mipangilio ya iPhone > Muda wa Skrini > Vikwazo vya Maudhui na Faragha.
Ikiwa bado WhatsApp haipatikani au haipo, huenda ukahitaji kurejesha simu yako. Tafadhali tembelea tovuti ya Msaada wa Apple kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuhifadhi nakala na kurejesha maelezo yako.
Ikiwa hutapea WhatsApp ruhusa ya kuzifikia anwani kwenye simu yako, bado utaweza:
 • Kupokea ujumbe kutoka kwa watumiaji wengine wa WhatsApp na vikundi.
 • Kubadili mipangilio ya WhatsApp.
Hutaweza:
 • Kuona majina yoyote, utaona tu namba za simu.
 • Kuanzisha Vikundi vipya au Orodha mpya za Matangazo.
Kutoonekana kwa anwani
Ikiwa huoni baadhi ya anwani kwenye WhatsApp, jaribu yafuatayo:
Kwa anwani za kimataifa:
Ikiwa anwani ambazo hazionekani zimehifadhiwa kwenye akaunti ya Exchange, huenda msimamizi wa akaunti yako hajaruhusu WhatsApp au programu zingine kufikia anwani zako. Unaweza kusuluhisha hali hii kwa:
 • Kunakili anwani zako zilizo kwenye akaunti ya Exchange katika kitabu cha anwani cha simu yako au iCloud.
 • Kumwomba msimamizi wako wa TEHAMA afanye WhatsApp iwe programu inayosimamiwa kwenye iPhone yako.
Kumbuka:
 • Kuna uwezekano kwamba akaunti za Exchange ni akaunti za kazi.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La