Jinsi ya kutaja mhusika kwenye kikundi

Ikiwa upo kwenye kikundi na mtu fulani, unaweza kumtaja kwenye ujumbe kwa kuandika alama ya “@” na kuchagua jina la mwasiliani kwenye orodha. Unapomtaja mtu, ataona arifa ya alama ya “@” katika orodha ya soga zake kando ya ujumbe ambao hajausoma.

Kumbuka: Kumtaja mtu kwenye kikundi kutafuta hatua yoyote ya mwasiliani kunyamazisha arifa za soga ya kikundi, isipokuwa kama amenyamazisha soga zako binafsi.
Ikiwa umetajwa kwenye kikundi
Utaona arifa ya alama ya “@” katika orodha ya soga zako kando ya ujumbe ambao hujausoma ikiwa mtu ametumia @ kukutaja au mtu amejibu ujumbe wako. Unapogusa soga hiyo, unaweza kupata kwa haraka ujumbe ulimotajwa au kujibu kwa kugusa kitufe "@" kinachoonekana kwenye kona ya chini ya kikundi.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La