Jinsi ya kutumia kusubiri simu

Android
iPhone
Ikiwa mtu anajaribu kukupiga simu kwenye WhatsApp wakati upo kwenye simu ya sauti au video ya WhatsApp, utapokea arifa kulingana na aina ya simu, na unaweza kuchagua kujibu au kukataa simu. Hii haitasumbua simu uliyonayo.
Mtu akikupigia simu kwenye WhatsApp
Unaweza kuchagua kutoka kwa hiari zifuatazo:
  • Maliza na Kubali: Maliza simu uliyonayo na kubali simu inayoingia.
  • Kataa: Kataa simu inayoingia na baki kwenye simu uliyonayo.
Mtu akikupigia simu nje ya WhatsApp
Ikiwa mtu anajaribu kukupigia simu kwa kupitia simu ya mezani au ya rununu nje ya WhatsApp wakati upo kwenye simu ya WhatsApp ya sauti au video, unaweza kugusa:
  • Jibu: Maliza simu uliyonayo na kubali simu inayoingia.
  • Kataa: Kataa simu inayoingia na baki kwenye simu uliyonayo.
  • Chunguza simu: Acha Msaidizi wa Google achunguze simu yako, na aulize nani anapiga simu na kwanini.
Kumbuka:
  • Kutegemeana na mtoa huduma wako, unaweza kupata gharama za simu zilizopigwa nje ya WhatsApp. Unaweza pia kupokea gharama aa simu za sauti au video zilizopigwa kwa kutumia WhatsApp, ikiwa unatumia data ya kuranda au umezidisha kikomo chako cha data.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La