Jinsi ya kuweka mipangilio ya kupakua kiotomatiki

Kwa kawaida, WhatsApp hupakua kiotomatiki picha kupitia muunganisho wako wa mtandao wa simu ili kukuwezasha kupata picha zako za hivi karibuni kwa haraka.

Ili uweke mipangilio ya kupakua picha, video au sauti, kiotomatiki nenda tu kwenye WhatsApp > gusa Hiari zaidi
> Mipangilio > Hifadhi na data > Upakuaji kiotomatiki wa midia.
Ukiwa hapo unaweza kuchagua ni wakati WhatsApp itapakua midia kiotomatiki.
Kumbuka: WhatsApp inajiunga na huduma zingine kupunguza uwezekano wa msongamano kwenye mtandao wakati wa janga la virusi vya korona (COVID-19). Ili kusaidia kuboresha kipimo data cha mtandao wa simu, tumezima upakuaji kiotomatiki wa nyaraka, video na ujumbe wa sauti katika baadhi ya maeneo.
Unapotumia data ya rununu
Midia uliyochagua yatapakuliwa kiotomatiki ukiwa unatumia data ya mtandao wa simu.
Unapotumia Wi-Fi
Midia uliyochagua yatapakuliwa kiotomatiki ukiwa unatumia Wi-Fi.
Unapotumia mtandao wa ng'ambo
Midia uliyochagua yatapakuliwa kiotomatiki ukiwa unatumia mtandao wa ng'ambo.
Kumbuka: Kuwasha upakuaji kiotomatiki unapotumia mtandao wa ng'ambo kunaweza kufanya utozwe gharama kubwa na mtoa huduma wako wa simu kwa sababu kwa kawaida utumiaji wa data ya mtandao mwingine huwa ghali.
Midia yanayopakuliwa kiotomatiki yatawekwa kwenye matunzio yako. Ukitaka kuzuia midia yote ya WhatsApp isionekane kwenye matunzio yako, tunapendekeza uunde faili au folda ya .nomedia ndani ya folda ya picha, sauti na video. Unaweza kufanya hivi kwa kutumia zana ya kufungua faili kutoka kwenye Duka la Google Play. Ukighairi baadaye, unaweza tu kufuta faili ya .nomedia halafu midia ya WhatsApp yataonekana tena kwenye matunzio yako.
Rasilimali zinazohusiana:
Jinsi ya kuweka mipangilio ya kupakua kiotomatiki kwenye: iPhone
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La