Imeshindwa kuunda au kurejesha nakala rudufu ya iCloud

iPhone
Ikiwa unakabiliwa na hitilafu wakati wa kuunda nakala au kurejesha kutoka iCloud, jaribu hatua za utatuzi zilizo hapa chini.
Kushindwa kuunda nakala
Ikiwa imeshindwa kuunda nakala kwenye iCloud:
 • Thibitisha kuwa umeingia katika akaunti ukitumia Kitambulisho cha Apple unachotumia kuingia kwenye iCloud.
 • Thibitisha kuwa iCloud Drive imewashwa. Nenda kwenye Mipangilio ya iPhone > gusa jina lako > iCloud > hakikisha kwamba iCloud Drive yako imewashwa.
 • Zima iCloud Drive kisha uiwashe tena. Nenda kwenye Mipangilio ya iPhone > gusa jina lako > iCloud > zima na uwashe iCloud Drive.
 • Ikiwa umewasha iCloud Drive kwenye kifaa chochote kwa kutumia Kitambulisho chako cha Apple, sasisha upate toleo la iOS 12 au jipya zaidi ili kuhifadhi nakala.
 • Thibitisha kuwa una nafasi ya kutosha kwenye akaunti yako ya iCloud ili kuunda nakala. Unahitaji angalau mara 2.05 zaidi ya nafasi kwenye akaunti yako ya iCloud kuliko nafasi halisi ya nakala yako.
 • Ikiwa unajaribu kuunda nakala ukitumia data ya mtandao wa simu, ruhusu utumiaji wa data ya mtandao wa simu kwa iCloud.
 • Tekeleza uwekaji wa nakala mwenyewe kwa kwenda kwenye WhatsApp Mipangilio > Soga > Nakala ya Soga > Hifadhi Nakala Sasa.
 • Jaribu kuhifadhi nakala mwenyewe kwenye mtandao tofauti. Hasa mtandao unaotumia zaidi.
Imeshindwa kurejesha nakala
Ikiwa umeshindwa kurejesha nakala iliyo kwenye iCloud:
 • Thibitisha kuwa unajaribu kurejesha data kwa kutumia nambari ya simu sawa na akaunti ya iCloud ambapo nakala iliundwa.
 • Kama unarejesha nakala iliyofumbwa mwisho hadi mwisho, unatumia nenosiri au ufunguo sahihi.
 • Thibitisha kuna nafasi ya kutosha kwenye iPhone yako ili kurejesha nakala hiyo. Unahitaji angalau mara 2.05 ya nafasi kwenye akaunti yako ya iCloud na kwenye simu yako kuliko ukubwa kamili wa nakala yako.
 • Ikiwa nakala iliundwa kwa kutumia iCloud Drive, utaweza tu kurejesha nakala kwenye iPhone iliyo na toleo la iOS 12 au jipya zaidi.
 • Ikiwa umewasha iCloud Drive kwenye kifaa chochote kwa kutumia Kitambulisho chako cha Apple, hutaweza kurejesha data kwenye iPhone yako isipokuwa kama ina toleo la iOS 12 au jipya zaidi.
 • Jaribu kurejesha ukitumia mtandao tofauti. Hasa mtandao unaotumia zaidi.
 • Zima iCloud Drive kisha uiwashe tena. Nenda kwenye Mipangilio ya iPhone > gusa jina lako > iCloud > zima na uwashe iCloud Drive.
 • Ondoka kwenye akaunti ya iCloud na uzime kisha uwashe iPhone yako. Kisha, ingia katika akaunti ya iCloud tena na ujaribu kurejesha tena.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La