Jinsi ya kuwasha au kuzima ujumbe unaotoweka kwenye kikundi

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Unaweza kutuma ujumbe unaotoweka kwenye WhatsApp kwa kuwasha hali ya ujumbe unaotoweka. Unaweza kuchagua ujumbe utoweke baada ya saa 24, siku 7 au siku 90. Unaweza kuwasha ujumbe unaotoweka kwa soga kadhaa zilizopo, ujumbe mpya unaotumwa kwenye soga hizo utatoweka baada ya muda uliochagua. Ujumbe uliotumwa au kupokelewa kabla ya kuwasha hali ya ujumbe unaotoweka hautaathiriwa.
Kuwasha ujumbe unaotoweka
Kwenye soga ya kikundi, washiriki wowote wa kikundi wanaweza kuwasha ujumbe unaotoweka. Hata hivyo, msimamizi wa kikundi anaweza kubadilisha mipangilio ya kikundi ili kuruhusu wasimamizi tu kuwasha hali ya ujumbe unaotoweka. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kubadilisha mipangilio ya usimamizi wa kikundi katika makala haya.
 1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp.
 2. Bofya jina la kikundi.
 3. Bofya Ujumbe Unaotoweka.
  • Unapoulizwa, bofya Endelea.
 4. Chagua Saa 24, Siku 7, au Siku 90.
 5. Chagua ni soga zipi unataka kuziwashia kipengele.
 6. Gusa
Pia unaweza kuwasha hali ya ujumbe unaotoweka wakati unaanzisha soga mpya ya kikundi.
Kuzima ujumbe unaotoweka
Mtu yeyote katika soga ya kikundi anaweza kuzima ujumbe unaotoweka wakati wowote, isipokuwa kama msimamizi wa kikundi amewaachia wasimamizi pekee uwezo huo.
 1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp.
 2. Bofya jina la kikundi.
 3. Bofya Ujumbe Unaotoweka.
  • Unapoulizwa, bofya Endelea.
 4. Chagua Zima.
 5. Chagua ni soga zipi unazotaka kuzizimia kipengele.
 6. Gusa
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La