Matatizo ya kutuma au kupokea ujumbe

Jambo ambalo kwa kawaida husababisha kutoweza kutuma au kupokea ujumbe wa WhatsApp ni muunganisho mbaya wa intaneti. Pata maelezo ya jinsi ya kutatua matatizo ya muunganisho kwenye: Android | iPhone
Ikiwa una uhakika kuwa simu yako imeunganishwa kwenye intaneti, kuna sababu chache zinazoweza kufanya ujumbe wa WhatsApp usitumwa:
  • Simu yako inahitaji kuanzishwa upya au kuzimwa na kuwashwa upya.
  • Mtu unayewasiliana naye amezuia nambari yako. Pata maelezo zaidi kwenye makala haya.
  • Hujakamilisha mchakato wa awali wa uthibitisho. Pata maelezo kuhusu uthibitisho kwenye: Android | iPhone.
  • Nambari ya unayejaribu kumtumia ujumbe kwenye WhatsApp haijahifadhiwa kwa usahihi kwenye simu yako. Pata maelezo kuhusu mfumo sahihi wa kila nambari ya simu hapa.

Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La