Jinsi ya kutuma ujumbe wa sauti

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Ujumbe wa sauti kwenye WhatsApp hukuruhusu kuwasiliana papo hapo na watu pamoja na vikundi. Unaweza kuutumia kuwasilisha taarifa muhimu na za haraka. Kwa hivyo, ujumbe wote wa sauti hupakuliwa kiotomatiki.

Kutuma ujumbe wa sauti
 1. Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
 2. Gusa na ushikilie maikrofoni
  halafu uanze kuzungumza.
 3. Mara unapomaliza, ondoa kidole chako kwenye maikrofoni
  . Ujumbe wa sauti utatumwa kiotomatiki.
Wakati unanakili ujumbe wa sauti, unaweza kutelezesha kidole kushoto ili kughairi.
Kutuma ujumbe mrefu zaidi wa sauti
 1. Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
 2. Gusa na ushikilie maikrofoni
  halafu uanze kuzungumza.
 3. Telezesha kidole juu ili uanze kurekodi bila kushikilia.
Unaweza pia kugusa kitufe chekundu cha kusitisha
ili usitishe kunakili au uhakiki rasimu ya ujumbe wako. Gusa aikoni nyekundu ya maikrofoni
ili kuendelea kunakili kwenye ujumbe huo huo wa sauti.
Kwenye ujumbe wa sauti uliotumwa utaona:
 • Maikrofoni ya kijivu
  kwa ujumbe wa sauti ambao haujachezwa na wapokeaji wote (lakini unaweza kuwa umechezwa na baadhi).
 • Maikrofoni ya bluu
  kwa ujumbe wa sauti ambao wapokeaji wote wameucheza.
Kumbuka: Kwenye baadhi ya simu, huenda itakubidi usubiri sekunde moja kabla ya kuzungumza ikiwa mwanzo wa ujumbe wako haurekodiwi.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La