Jinsi ya kuhariri jalada lako la biashara

Jalada lako la biashara linakuruhusu kuongeza maelezo kuhusu kampuni yako, ikiwa ni pamoja na jina la biashara yako, anwani, aina, maelezo, anwani ya barua pepe na tovuti. Watu wanaweza kuona maelezo haya kwa urahisi wanapoangalia jalada lako.
Ili uangalie jalada la biashara yako, fungua WhatsApp Web. Kisha, Bofya Menyu
> Jalada.
Kuhariri picha yako ya jalada
 1. Bofya aikoni ya picha yako ya jalada.
 2. Chagua mojawapo ya zifuatazo:
  • Angalia picha ili uone picha ya sasa ya jalada.
  • Piga picha ili upige picha mpya kwa kamera ya kompyuta yako.
  • Pakia picha ili upakie picha iliyopo kutoka kwenye faili zako.
  • Ondoa picha ili uondoe picha ya sasa ya jalada lako.
Kumbuka: Picha yako ya wasifu inaonekana hadharani kwa chaguomsingi. Pata maelezo ya jinsi ya kubadilisha mipangilio yako ya faragha kwenye makala haya.
Kuhariri picha yako ya jalada
 1. Bofya Hariri
  kwenye picha yako ya jalada.
 2. Chagua mojawapo ya zifuatazo:
  • Piga picha ili upige picha mpya kwa kamera ya kompyuta yako.
  • Pakia picha ili upakie picha iliyopo kutoka kwenye faili zako.
  • Ondoa picha ili uondoe picha ya sasa ya jalada.
Kumbuka: Picha yako ya wasifu inaonekana hadharani kwa chaguomsingi.
Kuhariri maelezo ya biashara yako
 1. Bofya Hariri
  kwenye sehemu ya Maelezo ya Biashara.
 2. Fanya masasisho yako.
 3. Bofya
  .
Kuhariri aina ya biashara yako
 1. Bofya Hariri
  katika sehemu ya kikundi.
 2. Chagua hadi aina tatu zinazofaa kwa ajili ya biashara yako.
 3. Bofya HIFADHI.
Kuhariri anwani ya biashara yako
 1. Bofya Hariri
  katika sehemu ya anwani.
 2. Weka anwani ya biashara yako.
 3. Bofya
  .
Kuhariri saa za kazi za biashara yako
 1. Bofya Hariri
  kwenye sehemu ya Anwani ya Biashara.
 2. Bofya kiolezo cha ratiba ambacho ungependa kutumia ili kuorodhesha saa zako:
  • SAA MAALUM: Tumia kisanduku cha kuteua ili kuchagua siku maalumu ambazo huwa unafungua. Unaweza pia kuonyesha vikundi maalumu vya muda ambapo huwa umefungua kila siku.
  • IMEFUNGULIWA WAKATI WOTE: Tumia kisanduku cha kuteua kuchagua siku maalumu ambazo huwa unafungua.
  • KWA MIADI TU: Tumia kisanduku cha kuteua ili kuchagua ni siku ipi ya juma biashara yako ipo wazi kupokea miadi.
 3. Bofya HIFADHI.
Kuhariri anwani yako ya barua pepe na tovuti
 1. Bofya Hariri
  katika sehemu unayotaka kusasisha.
 2. Sasisha taarifa zako.
 3. Bofya
  .
Kuhariri katalogi yako
 1. Bofya ANGALIA AU HARIRI KATALOGI ili kusasisha katalogi yako au kuunda mpya.
 2. Ongeza au hariri vitu kwenye katalogi yako unavyotaka. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuunda na kudumisha katalogi kwenye makala haya.
Kuhariri taarifa zilizo katika sehemu ya "Kukuhusu"
 1. Bofya Hariri
  katika sehemu ya Kuhusu.
 2. Sasisha taarifa zako.
 3. Bofya
  .
Kumbuka:
 • Jina la biashara yako, ramani ya eneo, namba ya simu na akaunti zilizounganishwa zinaweza tu kuhaririwa kwa kutumia programu ya WhatsApp Business kwenye kifaa cha mkononi.
Rasilimali zinazohusiana
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La