Unapoona ujumbe "Namba yako ya simu imepigwa marufuku kutumia WhatsApp. Wasiliana na kituo cha msaada ili upate usaidizi."
Ikiwa utapigwa marufuku, utapokea ujumbe ufuatao kwenye programu ya WhatsApp Business:
Namba yako ya simu imepigwa marufuku dhidi ya kutumia WhatsApp. Wasiliana na kituo cha msaada ili upate usaidizi.
Huwa tunapiga akaunti marufuku ikiwa tunaamini kuwa shughuli ya akaunti husika inakiuka Masharti yetu ya Huduma. Tafadhali kagua kwa umakini sehemu ya “Matumizi Yanayokubalika ya Huduma Zetu za Biashara” kwenye Masharti yetu ya Huduma ili upate maelezo zaidi kuhusu matumizi yanayofaa ya programu ya WhatsApp Business na shughuli zinazokiuka Masharti yetu ya Huduma.
Huenda tusitoe onyo kabla ya kupiga akaunti yako marufuku. Ikiwa unadhani kuwa akaunti yako imepigwa marufuku kimakosa, tafadhali tutumie barua pepe ili tuweze kushughulikia suala lako.