Kuhusu faragha ya hali

iPhone
Android
KaiOS
Masasisho yako za hali yanaweza tu kuonwa na mtu ikiwa una namba yake ya simu kwenye kitabu chako cha anwani na yeye ana namba yako ya simu kwenye kitabu chake cha anwani. Unaweza kuchagua kushiriki masasisho yako la hali na watu wote unaowasiliana nao, au wachache unaowachagua. Kwa kawaida, masasisho yako ya hali hushirikiwa na watu wote unaowasiliana nao.
Kubadilisha faragha ya hali yako
 1. Gusa Hali.
  • Android: Gusa Chaguo zaidi
   > Faragha ya hali.
  • iPhone: Gusa Faragha.
 2. Chagua mojawapo ya hiari zifuatazo:
  • Ninaowasiliana nao: Watu wote walio kwenye anwani zako wataona masasisho yako ya hali.
  • Ninaowasiliana nao isipokuwa...: Watu walio kwenye kitabu chako cha anwani pekee, isipokuwa wale unaowatenga, wataona masasisho yako ya hali.
  • Shirikisha tu na...: Ni watu walio kwenye kitabu chako cha anwani unaowachagua pekee ndio watakaoona masasisho yako ya hali.
Kumbuka:
 • Mabadiliko kwenye mipangilio yako ya faragha hayataathiri masasisho ya hali ambayo tayari umeyatuma.
 • Kama umezima taarifa za kusomwa, hutaweza kuona ni nani aliyeona masasisho yako ya hali. Ikiwa mtu unayewasiliana naye amezima taarifa za kusomwa, hutaweza kuona kama ameona masasisho yako ya hali.
Kushiriki masasisho ya hali kwenye Hadithi za Facebook na programu nyingine
Ukishiriki sasisho lako la hali, maudhui ya sasisho la hali yako yatashirikishwa na programu zingine. Unaposhiriki sasisho lako la hali, WhatsApp haitashiriki taarifa za akaunti yako na Facebook au programu nyinginezo.
Rasilimali zinazohusiana
 • Fahamu jinsi ya kutumia hali kwenye: Android | iPhone
 • Pata maelezo kuhusu jinsi ya kushiriki masasisho ya hali ya WhatsApp katika programu nyingine kwenye makala haya.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La