Jinsi ya kuthibitisha namba ya simu

Ni lazima uthibitishe namba yako ya simu ili kuanza kutumia WhatsApp.
Kuthibitisha namba ya simu:
 1. Fungua WhatsApp.
 2. Bonyeza Masharti & Faragha kusoma Masharti ya Huduma na Sera za Faragha.
 3. Bonyeza Kibali kukubali Masharti na endelea.
 4. Bonyeza Chagua nchi.
 5. Tafuta nchi au chagua nchi yako na bonyeza CHAGUA NCHI.
 6. ingiza namba yako ya simu.
 7. Bonyeza Mbele > SAWA kupokea msimbo wa uthibitishaji kwa SMS.
 8. Ingiza msimbo wa tarakimu-6 kutoka kwa SMS.
  • Ikiwa hukupokea msimbo, unaweza kubonyeza Tuma tena SMS au Nipigie simu kupigiwa simu na mfumo wa kiotomatiki ili kupewa msimbo.
 9. Ingiza jina lako. Tafadhali kumbuka:
  • Kikomo cha jina ni herufi 25.
  • Unaweza pia kuongeza Picha ya Jalada.
 10. Bonyeza Imekamilika.
Kumbuka: Video ifuatayo inawahusu tu watumiaji wa WhatsApp ambao wana JioPhone au JioPhone 2.

Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La