Â
Jinsi ya kuondoka na kufuta vikundi
Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Unaweza kufuta kikundi kwa washiriki wote wa kikundi ikiwa wewe ni msimamizi wa kikundi husika. Kabla ya kufuta kikundi ni sharti uwaondoe washiriki wote kwenye kikundi, kisha uondoke kwenye kikundi.
Unapofuta kikundi, hutakiona tena kwenye orodha ya soga zako na historia ya soga ya kikundi husika itafutwa kwenye simu yako. Washiriki wengine bado watakiona kikundi kwenye orodha ya soga zao. Hata hivyo, hamna atakayeweza kutuma ujumbe.
Kuondoa washiriki kwenye kikundi
- Fungua soga ya kikundi husika cha WhatsApp, kisha uguse jina la kikundi.
- Gusa jina la mshiriki > Ondoa kwenye Kikundi > Ondoa.
Kuondoka kwenye kikundi
Baada ya kuondoa washiriki wote kwenye kikundi, unahitaji kuondoka kwenye kikundi.
- Fungua soga ya kikundi husika cha WhatsApp, kisha uguse jina la kikundi.
- Au, telezesha kikundi kuelekea kushoto katika kichupo cha Soga. Kisha uguse Zaidi.
- Gusa Toka kwenye Kikundi > Toka kwenye Kikundi.
Kufuta kikundi
Baada ya kutoka kwenye kikundi, una chaguo ya kufuta kikundi hicho.
- Fungua soga ya kikundi husika cha WhatsApp, kisha uguse jina la kikundi.
- Au, telezesha kikundi kuelekea kushoto katika kichupo cha Soga. Kisha uguse Zaidi.
- Gusa Futa Kikundi > Futa Kikundi.