Jinsi ya kuondoka kwenye kikundi na kufuta vikundi

Android
iOS
KaiOS
Wavuti
Windows
Mac
Unaweza kufuta kikundi kwa washiriki wote ikiwa wewe ndiye msimamizi wa kikundi husika. Kabla ya kufuta kikundi ni sharti uwaondoe washiriki wote kwenye kikundi, kisha uondoke kwenye kikundi.

Kinachotokea unapoondoa mshiriki wa kikundi au kufuta kikundi

Unapofuta kikundi, hutaona kikundi husika kwenye orodha yako ya Soga. Pia, historia ya soga husika ya kikundi itafutwa kwenye simu yako.
Kumwondoa mshiriki au kufuta kikundi hakutafuta kikundi kwenye vifaa vya washiriki wengine. Washiriki wengine bado wataona kikundi katika orodha zao za Soga na wataona maudhui yote ya awali isipokuwa wao wenyewe wayafute. Hakuna atakayeweza kutuma ujumbe.
Haiwezekani kurejesha kikundi baada ya kufutwa.

Kuondoa washiriki wa kikundi

Kabla uweze kuondoka na kufuta kikundi, utatakiwa kuwaondoa washiriki wote wa kikundi.
  1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha uguse jina la kikundi.
  2. Gusa jina la mshiriki husika > Ondoa {member} > Sawa.

Kuondoka kwenye kikundi

Baada ya kuondoa washiriki wote kwenye kikundi, utahitaji kuondoka kwenye kikundi.
  1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha uguse jina la kikundi.
  2. Gusa Ondoka kwenye kikundi > Ondoka.
Unapoondoka kwenye kikundi, wasimamizi wa kikundi pekee ndiyo watakaoarifiwa.
Jina na namba yako ya simu itaonyeshwa kwenye sehemu ya Orodha ya washiriki wa zamani katika Maelezo ya kikundi. Huenda picha ya jalada lako ikaonyeshwa pia, kulingana na mipangilio yako.
Washiriki wa kikundi wanaweza kuona maelezo yako katika orodha hii kwa hadi siku 60 baada ya kuondoka kwenye kikundi.
Kumbuka: Ikiwa wewe ni msimamizi pekee wa kikundi na ukaondoka kwenye kikundi, mshiriki mwingine anachaguliwa bila utaratibu maalum kuwa msimamizi mpya. Ukijiunga tena na kikundi na ungependa kuwa msimamizi tena, unahitaji kumwomba msimamizi wa kikundi akufanye kuwa msimamizi.

Kufuta kikundi

Baada ya kuwaondoa washiriki wote na kutoka kwenye kikundi, una chaguo ya kufuta kikundi hicho.
  1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha uguse jina la kikundi.
  2. Gusa aikoni ya Futa kikundi > Futa kikundi.
    • Ikiwa hungependa kufuta maudhui ya kikundi kwenye simu yako, ondoa uteuzi wa Futa maudhui kwenye soga hii au Futa maudhui kwenye soga hizi.

Kufuta kikundi ambacho ni sehemu ya jumuiya

Vikundi ambavyo ni sehemu ya jumuiya havipo katika orodha yako ya Soga.
Baadhi ya njia za kupata jumuiya ni:
  • Kwenye kichupo cha Jumuiya.
  • Kwenye kichupo cha Soga.
  • Kwa kuandika jina la kikundi kwenye sehemu ya kutafutia.
Fuata hatua zilizo hapo juu ili ufute kikundi. Unaweza pia kuondoa kikundi kwenye jumuiya. Pata maelezo ya jinsi ya kufanya hivyo kwenye makala haya.

Je, hili linajibu swali lako?

Ndiyo
La