Jinsi ya kubadilisha namba yako ya simu

Android
iPhone

Kipengele cha kubadilisha namba yako ya simu kinakuruhusu kubadilisha namba ya simu inayohusishwa na akaunti yako ya WhatsApp kwenye simu hiyohiyo au mpya. Kabla ya kubadilisha namba yako ya simu:
 • Hakikisha kuwa namba yako mpya ya simu inaweza kupokea SMS au simu na ina muunganisho amilifu wa selula.
 • Hakikisha kuwa namba yako ya zamani ya simu sasa imesajiliwa kwenye WhatsApp. Unaweza kutafuta namba yako ya simu iliyosajiliwa kwa kufungua WhatsApp, kisha uguse Chaguo zaidi > Mipangilio > gusa picha yako ya jalada.
 • Hakikisha unatumia namba ya simu inayoruhusiwa. Namba za simu zisizoruhusiwa haziwezi kusajiliwa kwenye WhatsApp, namba hizo ni pamoja na:
 • VoIP
 • Simu za mezani (Kumbuka: Simu za mezani zinakubaliwa tu kwenye programu ya WhatsApp Business)
 • Namba zisizolipiwa
 • Namba za kulipia unapopigia
 • Namba za ufikiaji wa jumla (UAN)
 • Namba za binafsi
Kubadilisha namba ya simu kwenye simu hiyo hiyo
Kama unabadilisha namba yako ya simu na unatumia simu hiyo hiyo, kwanza ingiza SIM kadi mpya yenye namba mpya ya simu kwenye simu yako.
 1. Fungua WhatsApp.
 2. Gusa Chaguo zaidi
  > Mipangilio > Akaunti > Badilisha namba > INAYOFUATA.
 3. Weka namba yako ya zamani ya simu katika sehemu ya kwanza na namba yako mpya ya simu katika sehemu ya pili, zote zikiwa katika mfumo kamili wa kimataifa.
 4. Gusa INAYOFUATA.
  • Ukiwasha Waarifu unaowasiliana nao, unaweza kuchagua kama unataka kuwaarifu Wote unaowasiliana nao, Nilio na soga nao au Maalum... Ukichagua Maalum..., utahitaji kutafuta au kuchagua watumiaji unaotaka kuwaarifu, kisha gusa tiki
   .
  • Vikundi vyako vya soga vitaarifiwa unapobadilisha namba yako ya simu bila kujali kama ulichagua kuwaarifu unaowasiliana nao.
 5. Gusa NIMEMALIZA.
 6. Kisha utaombwa usajili namba yako mpya ya simu. Jifunze zaidi kwenye makala haya.
Kubadilisha namba ya simu kwenye simu mpya
Kama unahitaji kuhamisha historia yako ya soga, utahitaji kuunda chelezo la Google Drive kwenye simu yako ya zamani. Jifunze jinsi kwenye makala haya. Kama huundi chelezo kwa kutumia Google Drive, utahitaji kuhamisha chelezo lako kwa mkono, unaweza kujifunza jinsi ya kufanya hivyo kwenye makala haya.
Baada ya kubadilisha namba yako ya simu kwenye simu yako ya zamani:
 1. Sakinisha WhatsApp kwenye simu yako mpya.
 2. Sajili namba yako mpya ya simu.
 3. Rejesha nakala ya soga zako.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La