Kuhusu gharama za WhatsApp

Android
iOS
Hatutozi kwa kutuma ujumbe na maudhui au kupiga simu za sauti na video kwenye WhatsApp.
WhatsApp iliacha kutoza ada za usajili mwaka wa 2016.
Unahitaji kuwa na muunganisho wa intaneti kupitia data ya kifaa cha mkononi au Wi-Fi ili uweze kutumia WhatsApp. Unaweza kutozwa gharama za data kwa huduma hizi. Ili upate maelezo kuhusu gharama za data, tafadhali wasiliana na kampuni inayokupa huduma za simu ya mkononi.
Huenda pia gharama za data zikatumika iwapo unaranda au unatumia utumaji ujumbe chaguomsingi wa kifaa chako au mfumo wa kupiga simu.
Kwa mfano:
  • Ulituma mialiko kwa unaowasiliana nao (kupitia SMS/MMS) ili wajiunge na WhatsApp.
  • Ulikuwa unawatumia SMS/MMS watu wasio na akaunti ya WhatsApp. Wewe na unayewasiliana naye lazima muwe na WhatsApp kwenye vifaa vyenu ili kutuma na kupokea ujumbe na maudhui bila malipo kupitia WhatsApp.
Unaweza kufuatilia matumizi yako ya data ya WhatsApp kwenye Mipangilio.
Ili uone kiasi cha data uliyotumia:
  1. Gusa
    more options
  2. Gusa Mipangilio > Hifadhi na data.
  3. Gusa Matumizi ya mtandao.

Rasilimali zinazohusiana:

Je, hili linajibu swali lako?

Ndiyo
La