Jinsi ya kuangalia katalogi

Unaweza kuangalia bidhaa au huduma za biashara kwenye katalogi ya biashara hiyo. Ikiwa zina katalogi, unaweza kuipata kwenye jalada la biashara husika.
Kuangalia katalogi ya biashara
  1. Fungua soga kati yako na biashara.
  2. Gusa jina la biashara ili uone jalada la biashara hiyo kwenye WhatsApp Business.
  3. Gusa ANGALIA ZOTE karibu na KATALOGI.
Pia, ikiwa biashara ina katalogi inayotumika, unaweza kugusa kitufe cha ununuzi (
kwenye Android au
kwenye iPhone) katika soga kati yako na biashara ili ufikie katalogi ya biashara hiyo moja kwa moja.
Ili ushiriki katalogi nzima au bidhaa mahususi, gusa aikoni ya kiungo kisha uchague mojawapo ya yafuatayo:
  • Tuma kiungo kupitia WhatsApp: hushiriki kiungo cha bidhaa au katalogi iliyochaguliwa na wengine kupitia WhatsApp
  • Nakili kiungo: hunakili kiungo
  • Shiriki kiungo: hushiriki bidhaa au katalogi iliyochaguliwa kupitia barua pepe au programu za kutuma ujumbe
Rasilimali zinazohusiana
Jinsi ya kushiriki bidhaa au huduma kwenye katalogi: Android | iPhone | Web na Desktop
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La