Jinsi ya kufanya mabadiliko kwenye vikundi

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Kwa kawaida, mshiriki yeyote wa kikundi anaweza kubadili mada, aikoni, maelezo ya kikundi au kutuma ujumbe. Hata hivyo, msimamizi wa kikundi anaweza kubadili mipangilio ya kikundi ili kuruhusu wasimamizi pekee kuhariri maelezo ya kikundi au kuidhinisha washiriki wapya.
Kubadilisha maelezo ya kikundi
Kubadili mada ya kikundi
 1. Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp, kisha bofya mada ya kikundi.
  • Vinginevyo, bofya Menyu (
   au
   ) katika kona ya juu ya > Maelezo ya kikundi.
 2. Bofya Hariri
  upande wa kulia wa jina la kikundi.
 3. Weka mada mpya, kisha bofya alama ya tiki ya kijivu
  ili uhifadhi.
  • Ukomo wa mada ni herufi 25.
  • Unaweza kuweka emoji kwenye jina lako kwa kubofya aikoni ya Emoji
   .
Kubadilisha aikoni ya kikundi
 1. Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp, kisha bofya mada ya kikundi.
  • Vinginevyo, bofya Menyu (
   au
   ) katika kona ya juu ya > Maelezo ya kikundi.
 2. Elekeza juu ya aikoni, kisha ubofye BADILI AIKONI YA KIKUNDI
  .
 3. Chagua Kuangalia picha, Kupiga picha, Kupakia picha, Emoji na Kibandiko au Tafuta kwenye Wavuti ili uweke picha au Ondoa picha. Kipengele cha Tafuta kwenye Wavuti kinapatikana tu kwenye WhatsApp Desktop.
Kubadilisha maelezo ya kikundi
 1. Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp, kisha bofya mada ya kikundi.
  • Vinginevyo, bofya Menyu (
   au
   ) katika kona ya juu ya > Maelezo ya kikundi.
 2. Bofya Hariri
  upande wa kulia wa maelezo ya kikundi.
 3. Weka maelezo mapya, kisha ubofye alama ya uhakiki ya kijivu
  ili kuhifadhi.
  • Unaweza kuweka emoji kwenye maelezo yako kwa kubofya aikoni ya Emoji
   .
Idhinisha washiriki wapya kama msimamizi wa kikundi
Ikiwa kipengele cha Idhinisha Washiriki Wapya kimewashwa kwenye Mipangilio ya Kikundi, wasimamizi lazima waidhinishe mtu yeyote anayetaka kujiunga kwenye kikundi.
 1. Kwenye kichupo cha Soga, chini ya jina la kikundi kutakuwa na arifa ikiwa kuna maombi ambayo yanasubiri.
 2. Bofya ujumbe wa maombi yanayosubiri ili kufikia Washiriki wanaosubiri.
 3. Ikiwa utaidhinisha mtu, ataongezwa kwenye kikundi. Ikiwa utaondoa ombi lake, hataongezwa.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La