Â
Jinsi ya kufanya mabadiliko kwenye vikundi
Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Kwa chaguomsingi, mshiriki yeyote wa kikundi anaweza kubadili aikoni, jina au maelezo. Hata hivyo, msimamizi wa kikundi anaweza kubadili mipangilio ya kikundi ili kuruhusu wasimamizi pekee kuhariri maelezo ya kikundi.
Kubadili maelezo ya kikundi
Kubadili jina la kikundi
- Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha ubofye Chaguo > Maelezo ya kikundi > Sawa.
- Chagua jina la kikundi, kisha ubonyeze Hariri.
- Weka jina jipya, kisha ubonyeze Hifadhi.
- Jina lisizidi herufi 100.
Ili kubadili aikoni ya kikundi
- Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha ubofye Chaguo > Maelezo ya kikundi > Sawa.
- Chagua aikoni ya kikundi, kisha ubonyeze Chaguo.
- Bonyeza Chagua picha kisha uchague kwenye Kamera au Matunzio ili uweke picha.
- Bonyeza Nimemaliza.
Kubadili maelezo ya kikundi
- Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp, kisha ubonyeze Chaguo > Maelezo ya kikundi.
- Chagua maelezo ya kikundi, kisha ubonyeze Hariri.
- Weka maelezo mapya, kisha ubonyeze Hifadhi.
Rasilimali zinazohusiana: