Jinsi ya kufanya mabadiliko kwenye vikundi

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Mac
Kwa chaguomsingi, mshiriki yeyote wa kikundi anaweza kubadilisha jina, aikoni, maelezo ya kikundi au kutuma ujumbe. Hata hivyo, msimamizi wa kikundi anaweza kubadilisha mipangilio ya kikundi ili kuruhusu wasimamizi pekee kuhariri maelezo ya kikundi au kuidhinisha washiriki wapya. Ili kutambua msimamizi wa kikundi ni nani, gusa jina husika la kikundi kisha utafute Msimamizi karibu na jina la anwani.
Kubadilisha maelezo ya kikundi
Kubadilisha maelezo ya kikundi
  1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha uguse jina la kikundi.
  2. Gusa maelezo yaliyopo au uguse Weka Maelezo ya Kikundi.
  3. Weka maelezo mapya, kisha uguse Hifadhi.
Kubadili aikoni ya kikundi
  1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha uguse jina la kikundi.
  2. Gusa Hariri > Weka Picha.
  3. Chagua Piga Picha, Chagua Picha, Emoji na Kibandiko au Tafuta kwenye Wavuti ili uweke picha mpya.
  4. Baada ya kuchagua picha yako, gusa Nimemaliza.
Kuidhinisha washiriki wapya ukiwa wasimamizi wa kikundi
Ikiwa kipengele cha Idhinisha Washiriki Wapya kimewashwa kwenye Mipangilio ya Kikundi, ni lazima wasimamizi waidhinishe mtu yeyote ambaye angependa kujiunga kwenye kikundi.
  1. Kwenye kichupo cha Soga, chini ya jina la kikundi kutakuwa na arifa ya Kukagua maombi yanayosubiri kujiunga kwenye kikundi.
  2. Gusa Kagua ili uangalie orodha ya maombi yanayosubiri.
  3. Karibu na jina la mshiriki anayesubiri, gusa alama ya tiki ili uidhinishe ombi au uguse X ili ukatae ombi husika. Kumbuka: Ikiwa utaidhinisha mtu, ataongezwa kwenye kikundi. Ikiwa utatupilia mbali ombi lake, hataongezwa.
Rasilimali zinazohusiana
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La