Jinsi ya kufanya mabadiliko kwenye vikundi

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Kwa chaguomsingi, mshiriki yeyote wa kikundi anaweza kubadili mada, aikoni, maelezo ya kikundi au kutuma ujumbe. Hata hivyo, msimamizi anaweza kubadili mipangilio ya kikundi ili kuruhusu wasimamizi pekee kuhariri maelezo ya kikundi.
Kubadili maelezo ya kikundi
Kubadili mada ya kikundi
 1. Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp, kisha ubofye mada ya kikundi.
  • Au, bofya Menyu (
   au
   ) kwenye kona ya juu > Maelezo ya kikundi.
 2. Bofya Hariri
  iliyo upande wa kulia wa mada ya kikundi.
 3. Weka mada mpya, kisha bofya alama ya tiki ya kijivu
  ili uhifadhi.
  • Ukomo wa mada ni herufi 25.
  • Unaweza kuweka emoji kwenye mada yako kwa kubofya aikoni ya Emoji
   .
Kubadili aikoni ya kikundi
 1. Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp, kisha ubofye mada ya kikundi.
  • Au, bofya Menyu (
   au
   ) kwenye kona ya juu > Maelezo ya kikundi.
 2. Fanya kiashiria kielee juu ya aikoni, kisha bofya BADILISHA AIKONI YA KIKUNDI
  .
 3. Chagua Kutazama picha, Kupiga picha, Kupakia picha, au Kutafuta kwenye Wavuti ili kuweka picha mpya au Kuondoa picha. Kutafuta kwenye Wavuti kunapatikana kwenye WhatsApp Desktop pekee.
Kubadili maelezo ya kikundi
 1. Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp, kisha ubofye mada ya kikundi.
  • Au, bofya Menyu (
   au
   ) kwenye kona ya juu > Maelezo ya kikundi.
 2. Bofya Hariri
  iliyo upande wa kulia wa maelezo ya kikundi.
 3. Weka maelezo mapya, kisha bofya alama ya tiki ya kijivu
  ili uhifadhi.
  • Unaweza kuweka emoji kwenye maelezo yako kwa kubofya aikoni ya Emoji
   .
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La