Jinsi ya kuweka mipangilio ya kupakua kiotomatiki

Kwa kawaida, WhatsApp hupakua kiotomatiki picha kupitia muunganisho wako wa mtandao wa simu ili kukuwezasha kupata picha zako za hivi karibuni kwa haraka. Sauti na video hupakuliwa kiotomatiki kwenye Wi-Fi pekee.

Unaweza kudhibiti mapendeleo yako kwa kufungua WhatsApp > Mipangilio > Hifadhi na Data. Ukiwa hapo unaweza kuchagua wakati WhatsApp itapakua picha, sauti, video na nyaraka kiotomatiki. Gusa kila aina ya midia kisha uchague Kamwe, Wi-Fi, au Wi-Fi na Data ya Simu.
Kumbuka: WhatsApp inajiunga na huduma zingine kupunguza uwezekano wa msongamano kwenye mtandao wakati wa janga la virusi vya korona (COVID-19). Ili kusaidia kuboresha kipimo data cha mtandao wa simu, tumezima upakuaji otomatiki wa nyaraka, video na ujumbe wa sauti katika baadhi ya maeneo.
Kamwe
Midia haitapakuliwa kiotomatiki kamwe. Utahitajika kugusa kila faili ili uipakue.
Kumbuka: Ukiweka mipangilio yako ya Pakua Kiotomatiki iwe Kamwe, video zako hazitapakuliwa kiotomatiki. Hata hivyo, mara tu unapogusa kitufe cha kucheza, video itaanza kucheza papo hapo na kuendelea na mchakato wa kupakuliwa chinichini.
Wi-Fi
Midia itapakuliwa kiotomatiki unapounganishwa kwenye mtandapepe wa Wi-Fi kama vile intaneti yako ya nyumbani.
Wi-Fi na Data ya Simu
Midia itapakuliwa kiotomatiki wakati wowote ukiwa na muunganisho wa intaneti.
Ikiwa una kifurushi cha data chenye ukomo, tunapendekeza uweke mipangilio ili midia ipakuliwe kiotomatiki wakati umeunganishwa kwenye Wi-Fi tu.
Rasilimali zinazohusiana:
Jinsi ya kuweka mipangilio ya kupakua kiotomatiki kwenye: Android
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La