Kushiriki viungo vya katalogi

Android
iOS
Katalogi huwaruhusu wateja kuvinjari bidhaa au huduma za biashara, kuuliza maswali na kuwasiliana na biashara. Wateja wanaweza kuchagua bidhaa au huduma wanayovutiwa nayo na kushiriki kwa marafiki zao au kutumia biashara ujumbe kuiuliza maswali.
Kushiriki bidhaa au huduma kutoka kwenye katalogi:
 1. Nenda kwenye Katalogi
 2. Chagua bidhaa au huduma ambayo ungependa kushiriki
 3. Gusa
  link
 4. Kisha unaweza kushiriki bidhaa kwenye katalogi yako na wanunuzi watarajiwa popote pale kwa kuchagua mojawapo ya chaguo hizi:
  • Tuma kiungo kupitia WhatsApp Business: Shiriki kiungo cha bidhaa ambayo umechagua kupitia WhatsApp
  • Nakili Kiungo
  • Shiriki Kiungo: Shiriki bidhaa ambayo umechagua kupitia barua pepe au programu zingine za kutuma ujumbe
 5. Chagua soga za vikundi au binafsi ambazo ungependa kushiriki nazo bidhaa au huduma
 6. Si lazima: Wekea mapendeleo ujumbe uliojumuishwa na kiungo ili ueleze vyema kipengee unachoshiriki.
 7. Gusa
  send
Kiungo utachoshiriki kitafungua bidhaa au katalogi moja kwa moja ikiwa mpokeaji atakifungua kwenye programu ya WhatsApp Messenger au WhatsApp Business.
Unaposhiriki kupitia barua pepe au kivinjari, kiteuzi kitamruhusu mtumiaji kuchagua jinsi ya kukifungua kiungo.
Kumbuka: Viungo vya katalogi ambavyo vinashirikiwa huenda vikose kufunguka ikiwa mpokeaji anatumia toleo la zamani kuliko toleo la Android 6.0
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La