Jinsi ya kuweka nakala rudufu kwenye Hifadhi ya Google

Android
Ili kuweka nakala rudufu kwenye Hifadhi ya Google, utahitaji:
 • Akaunti ya Google inayofanya kazi kwenye kifaa chako.
 • Huduma za Google Play iwe imesakinishwa kwenye kifaa chako. Hii ni programu inayotumika kusasisha programu za Google na programu kutoka kwenye Duka la Google Play.
 • Nafasi ya kutosha kwenye kifaa chako ili kuhifadhi nakala.
 • Muunganisho imara na thabiti wa intaneti.
Kuweka nakala rudufu kwenye Hifadhi ya Google
 1. Fungua WhatsApp.
 2. Gusa Chaguo zaidi
  > Mipangilio > Soga > Nakala ya soga > Weka nakala kwenye Hifadhi ya Google.
 3. Chagua marudio ya kuweka nakala badala ya kuchagua Kamwe.
 4. Chagua akaunti ya Google utakayotumia kuhifadhi nakala ya historia yako ya soga.
  • Ikiwa huna akaunti ya Google iliyounganishwa, gusa Ongeza akaunti unapoulizwa kuweka vitambulisho vyako vya kuingilia.
 5. Gusa Hifadhi nakala kupitia ili uchague mtandao unaotaka kuutumia kwa kuhifadhi nakala.
Kumbuka: Kuhifadhi nakala kupitia data ya mtandao wa simu kunaweza kukuongezea gharama za data.
Kuwasha uwekaji wa nakala iliyofumbwa mwisho hadi mwisho
Kwa safu ya ziada ya usalama, unaweza kuwasha ufumbaji wa mwisho hadi mwisho kwa nakala unayoweka kwenye Hifadhi ya Google.
 1. Fungua WhatsApp.
 2. Gusa Chaguo zaidi
  > Mipangilio > Soga > Nakala ya soga > Ufumbaji wa nakala mwisho hadi mwisho.
 3. Gusa WASHA.
 4. Unda nenosiri au tumia ufunguo wa ufumbaji wenye tarakimu 64.
 5. Gusa Unda ili uunde nakala iliyofumbwa mwisho hadi mwisho.
Kujiwekea nakala rudufu mwenyewe kwenye Hifadhi ya Google
Unaweza pia kuchagua kujiwekea nakala rudufu ya soga zako kwenye Hifadhi ya Google wakati wowote.
 1. Fungua WhatsApp.
 2. Gusa Chaguo zaidi
  > Mipangilio > Soga > Nakala ya soga > HIFADHI NAKALA.
Kuweka mipangilio yako ya nakala rudufu ya Hifadhi ya Google
Kubadili marudio ya kuweka nakala kwenye Hifadhi ya Google
 1. Fungua WhatsApp.
 2. Gusa Chaguo zaidi
  > Mipangilio > Soga > Nakala ya soga > Weka nakala kwenye Hifadhi ya Google.
 3. Chagua marudio ya kuhifadhi nakala.
Kubadilisha akaunti unayotaka kutumia kuhifadhi nakala
 1. Fungua WhatsApp.
 2. Gusa Chaguo zaidi
  > Mipangilio > Soga > Nakala ya soga > Akaunti ya Google.
 3. Chagua akaunti ya Google utakayotumia kuhifadhi nakala ya historia yako ya soga.
Kumbuka: Ukibadilisha akaunti yako ya Google, utapoteza ufikiaji wa nakala zozote rudufu ulizohifadhi kwenye akaunti yako.
Kubadilisha aina ya mtandao unaotaka kuutumia kuhifadhi nakala
 1. Fungua WhatsApp.
 2. Gusa Chaguo zaidi
  > Mipangilio > Soga > Nakala ya soga > Hifadhi nakala kupitia
 3. Chagua aina ya mtandao unaotaka kuutumia kuhifadhi nakala.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La