Kupokea msimbo wa uthibitisho bila kuuomba

Ili kulinda akaunti yako, WhatsApp itakutumia taarifa ya kusukuma wakati mtu anapojaribu kusajili akaunti ya WhatsApp kwa nambari yako ya simu. Ili kuweka akaunti yako salama, usishirikishe msimbo wako wa uthibitisho na wengine.
Unapopokea taarifa hii, inamaanisha kwamba mtu ameingiza nambari yako ya simu na kuomba msimbo wa usajili. Hii mara nyingi hutokea ikiwa mtumiaji mwingine anaingiza nambari yako kwa makosa wakati akijaribu kuingiza nambari yake mwenyewe kujisajili, na inaweza pia kutokea wakati mtu anajaribu kuchukua akaunti yako.
Usishirikishe msimbo wako wa uthibitisho wa WhatsApp na wengine. Ikiwa mtu anajaribu kuchukua akaunti yako, anahitaji msimbo wa uthibitisho uliotumwa kwa SMS kwa nambari yako ya simu ili kufanya hivyo. Bila msimbo huu, mtumiaji yeyote akijaribu kuthibitisha nambari yako hawezi kukamilisha mchakato wa uthibitisho na kutumia nambari yako ya simu kwenye WhatsApp. Hii inamaanisha kuwa umebaki na udhibiti wa akaunti yako ya WhatsApp.
Kumbuka
  • WhatsApp haina maelezo ya kutosha ya kumtambua mtu anayejaribu kuthibitisha akaunti yako ya WhatsApp.
  • WhatsApp imefumbwa mwisho hadi mwisho na ujumbe unahifadhiwa kwenye kifaa chako, kwa hivyo mtu ambaye anatumia akaunti yako kwenye kifaa kingine hawezi kusoma mazungumzo ya zamani.
Rasilimali
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La