Kuhusu viungo vinavyotiliwa shaka

Kwa baadhi ya viungo unavyopokea kwenye soga, unaweza kuona kiashirio cha kiungo kinachotiliwa shaka.
Kiashirio hiki kinaweza kuonekana wakati kiungo kina mchanganyiko wa herufi ambazo huchukuliwa kuwa si za kawaida. Matapeli wanaweza kutumia mchanganyiko wa herufi kukudanganya kugusa viungo unavyoweza kudhani vinaelekeza kwenye tovuti sahihi, lakini vikakupeleka kwenye tovuti ya kuhadaa.
Huu hapa mfano wa kiungo cha kutilia shaka:
https://ẉhatsapp.com/free-tickets
Kumbuka: Herufi ya kwanza inaonekana kama herufi "w" lakini badala yake ni herufi "ẉ", ina maana kwamba tapeli anaweza kuwa amekudanganya ukatembelea tovuti ambayo haihusiani na WhatsApp.
Unapopokea viungo, kagua kwa makini maudhui ya ujumbe huo. Kiungo kikiwa kimewekewa alama ya kutiliwa shaka, unaweza kukigusa halafu ujumbe ibukizi utatokea, ambao utaonyesha herufi zisizo za kawaida kwenye kiungo hicho. Kisha unaweza kuchagua kufungua kiungo au kurudi kwenye soga.
WhatsApp hufanya ukaguzi wa kiotomatiki kubaini ikiwa kiungo ni cha kutilia shaka. Ili kulinda faragha yako, ukaguzi huu hufanyika kikamilifu kwenye kifaa chako, na kwa sababu ya ufumbaji wa mwisho hadi mwisho, WhatsApp haiwezi kuona maudhui ya ujumbe wako.
Ili upate maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuwa salama kwenye WhatsApp, soma makala haya.
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La