Jinsi ya kupiga simu ya sauti

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Simu ya sauti hukuruhusu kuwapigia waasiliani wako simu ya bure kwa kutumia WhatsApp, hata kama upo nchi nyingine. Kupiga simu ya sauti kunatumia muunganisho wa intaneti wa simu yako badala ya kifurushi chako cha dakika za maongezi. Unaweza kutozwa ada za data.
Kupiga simu ya sauti
 1. Fungua soga ya binafsi na mtumiaji unayetaka kumpigia simu.
 2. Gusa Simu ya sauti
  .
Vinginevyo, fungua WhatsApp, kisha gusa kichupo cha Simu gusa > Simu Mpya
. Tafuta mtumiaji unayetaka kumpigia simu, kisha gusa Simu ya Sauti
.
Kupokea simu ya sauti
Kama simu yako imefungwa, utaona skrini ya Sauti ya WhatsApp... inaingia wakati mtu anakupigia simu, ambapo unaweza:
 • Kutelezesha kulia sogeza kujibu ili kujibu simu.
 • Kugusa Nikumbushe, kisha chagua kama unataka kukumbushwa Ninapoondoka au Ndani ya saa 1.
 • Kukataa simu kwa kubonyeza mara mbili kitufe cha kuwasha iliyopo pembeni mwa iPhone.
Kama hujafunga simu yako, utaona skrini ya Sauti ya WhatsApp... wakati mtu fulani anakupigia simu, ambapo unaweza:
 • Kugusa Kubali.
 • Kugusa Kataa.
 • Kugusa Nikumbushe, kisha chagua kama unataka kukumbushwa Ninapoondoka au Ndani ya saa 1.
 • Kugusa Ujumbe ili ukatae simu kwa kutuma ujumbe wa haraka.
Kubadilisha kati ya simu za sauti na simu za video
Kubadili kutoka simu ya sauti kuwa simu ya video
 1. Ukiwa kwenye simu ya sauti, gusa simu ya video
  > Badilisha.
 2. Mtumiaji unayempigia simu ataona ombi la kubadilisha kuwa simu ya video na anaweza kukubali au kukataa kubadilisha.
Kubadili kutoka kwa simu ya video kwenda kwa simu ya sauti
 1. Ukiwa kwenye simu ya video, gusa Zima Video
  , hali itakayomwarifu mtumiaji unayewasilianaye kwa simu ya video.
 2. Mara tu unayewasiliana naye akizima video yake, simu itabadilishwa na kuwa simu ya sauti.
Kumbuka:
 • Hakikisha kwamba wewe na unaowasiliana nao mna muunganisho wa Intaneti ulio imara wakati mnapiga au kupokea simu za video za kikundi. Ubora wa simu utategemea mtumiaji mwenye muunganisho hafifu.
 • Upigaji wa simu unapatikana kwenye iPhone zinazotumia iOS 12 au matoleo mapya zaidi.
 • Huwezi kufikia namba za huduma za dharura kupitia WhatsApp, kama vile 911 nchini Marekani. Kupiga simu za dharura, unapaswa kufanya mipango ya mawasiliano mbadala.
Rasilimali zinazohusiana:
 • Jinsi ya kupiga simu ya sauti ya kikundi kwenye: Android | iPhone
 • Jinsi ya kupiga simu ya sauti kwenye Android
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La