Kubadilisha ukubwa wa fonti

iPhone
Android
Windows
Unaweza kubadili ukubwa wa fonti kwenye soga za WhatsApp katika Mipangilio ya WhatsApp. Ukubwa wa herufi kwenye baadhi ya skrini katika programu unategemea mipangilio ya kifaa chako.
Kubadilisha ukubwa wa fonti kwenye soga
  1. Fungua WhatsApp.
  2. Gusa Chaguo zaidi
    .
  3. Gusa Mipangilio > Soga > Ukubwa wa fonti.
  4. Unaweza kuchagua kuanzia Ndogo, Wastani, au Kubwa.
Kubadilisha ukubwa wa mwandiko kwenye skrini nyingine
  1. Nenda kwenye Mipangilio ya kifaa.
  2. Gusa Ufikivu > Maandishi na onyesho.
  3. Gusa Ukubwa wa Fonti.
  4. Sogeza kitelezi ili urekebishe ukubwa wa fonti.
Kumbuka:
  • Fonti maalum haziwezi kutumika.
  • Maagizo yaliyoelezwa hapo juu yanaweza kutofautiana kulingana na simu yako. Tafadhali wasiliana na mtengenezaji wa simu yako kwa maagizo maalumu.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La