Jinsi ya kutuma maudhui

Android
iPhone
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Tuma picha, video, hati, vibandiko au anwani
 1. Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
 2. Bofya Ambatisha
  au
  , kisha ubofye:
  • Picha na Video
   ili uchague picha au video kutoka kwenye kompyuta yako. Unaweza kutuma hadi picha au video 30 kwa mara moja na kuweka manukuu kwa kila picha au video. Au, unaweza kuburura na kudondosha picha au video moja kwa moja katika sehemu ya maandishi. Kila video unayotuma isidizi MB 16.
  • Kamera
   ili upige picha kwa kutumia kamera ya kompyuta yako.
  • Hati
   ili uchague hati kwenye kompyuta yako. Vinginevyo, unaweza kuburuta na kudondosha hati moja kwa moja katika sehemu ya maandishi. Ukubwa wa hati unaoruhusiwa ni GB 2.
  • Anwani
   ili utume maelezo ya anwani zilizohifadhiwa kwenye kitabu cha anwani cha simu yako kwenye WhatsApp.
 3. Bofya Tuma
  au
  .
Kutuma ujumbe wa sauti
 1. Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
 2. Bofya maikrofoni
  au
  kisha uanze kuzungumza kwenye maikrofoni ya kompyuta yako.
 3. Baada ya kumaliza, bofya
  ili utume ujumbe wa sauti.
Kumbuka: Unaporekodi ujumbe wa sauti, unaweza kubofya Simamisha
ili usitishe kurekodi kwa muda na maikrofoni
au
uendelee kurekodi. Kughairi au kufuta rekodi yako, bofya
.
Kuhifadhi picha au video kwenye kompyuta
 1. Bofya picha au video unayotaka kuhifadhi.
 2. Bofya Pakua
  au
  . Ukiulizwa, bofya Hifadhi.
Rasilimali zinazohusiana:
Jinsi ya kutuma maudhui: Android | iPhone | KaiOS
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La