Jinsi ya kutuma maudhui

Android
iPhone
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows

Kutuma maudhui, hati, mahali, au anwani
 1. Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
 2. GusaAmbatisha
  . Kisha, gusa:
  • Kamera ili kupiga picha au kurekodi video mpya kwa kamera yako. Kumbuka: Video ambazo zimerekodiwa kwa kutumia WhatsApp zina ukomo wa MB 16.
  • Maktaba ya Picha na Video ili uchague picha au video kutoka kwenye picha za iPhone au albamu yako. Baada ya kuchagua picha au video, gusaWeka
   katika sehemu ya chini kushoto ili uchague picha au video kadhaa kwa wakati mmoja.
  • Hati ili uchague hati kwenye Hifadhi ya iCloud au programu nyingine kama vile Hifadhi ya Google, Dropbox, n.k. Kumbuka: Uwezo wa kutuma hati unapatikana tu kwa watumiaji wenye iOS 12 na matoleo mapya zaidi. Ukubwa wa faili unaoruhusiwa ni GB 2.
  • Mahali ili utume data ya mahali ulipo au eneo la karibu.
  • Unayewasiliana naye ili utume maelezo ya unayewasiliana naye. Kwa kawaida, maelezo yote yaliyohifadhiwa katika kitabu cha anwani cha simu kuhusu aliyechaguliwa yatashirikiwa. Gusa vipengee kwenye skrini ya Shiriki Anwani ili uondoe maelezo ambayo usingependa kuyashiriki.
 3. Unaweza pia kuongeza manukuu kwenye picha na video. Badili kati ya picha ili uongeze manukuu kwa kila mojawapo.
 4. Gusa Tuma
  .
Pia, unaweza kushiriki viungo kwenye Facebook au video za Instagram na zinaweza kucheza ndani ya WhatsApp. Onyesho la kukagua litajitokeza baada ya kubandika kiungo kwenye soga yako.
Kumbuka: Ili utume maudhui, hati, viungo, mahali au anwani, utahitaji kutoa ruhusa ya programu kufikia Huduma za Mahali za iPhone yako, Anwani, Picha na Kamera kwenye iPhone Mipangilio > Faragha.
Tuma maudhui yenye ubora wa juu
 1. Gusa Mipangilio ya WhatsApp.
 2. Gusa Hifadhi na data.
 3. Gusa Ubora wa Picha Unayopakia.
 4. Gusa Otomatiki (inapendekezwa), Ubora wa juu au Kiokoa data.
Kumbuka: Maudhui yenye ubora wa juu.
Kusambaza maudhui, hati, mahali au anwani
 1. Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
 2. Gusa na ushikilie aina ya ujumbe ambao ungependa kuusambaza, kisha uguse Sambaza. Unaweza kuchagua zaidi ya ujumbe mmoja.
 3. Gusa Sambaza
  .
 4. Chagua soga ambayo ungependa kusambazia ujumbe kisha gusa Sambaza.
Unaposambaza midia, nyaraka, mahali au waasiliani, huna haja ya kupakua tena. Ujumbe uliosambazwa ambao kwa asili haukutumwa na wewe utaonyesha lebo ya "Ulisambazwa".
Kumbuka: Manukuu hayatasambazwa kwenye maudhui.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La