Jinsi ya kutumia bofya kupiga soga

Kipengele cha WhatsApp cha bofya kupiga soga kinakuruhusu kuanzisha soga na mtu bila ya namba ya simu kuhifadhiwa kwenye kitabu chako cha anwani cha simu yako. Ilimradi unajua namba ya simu ya mtu huyu na ana akaunti ya WhatsApp inayofanya kazi, unaweza kuunda kiungo kinachokuwezesha kuanza kupiga soga naye. Kwa kubofya kiungo, soga na mtu huyo inafunguka kiotomatiki. Bofya kupiga soga hufanya kazi kote kwa simu yako na kwa WhatsApp Web.
Unda kiungo chako
Tumia https://wa.me/<number> ambapo <number> ni namba ya simu kamili katika muundo kwa kimataifa. Acha sufuri zozote, mabano, au vistari unapo ongeza namba ya simu katika muundo wa kimataifa.
Mifano:
Tumia: https://wa.me/1XXXXXXXXXX
Usitumie: https://wa.me/+001-(XXX)XXXXXXX
Unda kiungo chako na ujumbe uliojazwa mapema
Ujumbe uliojazwa mapema utaonekana kiotomatiki katika sehemu ya ujumbe kwenye soga. Tumia https://wa.m/whatsappphonenumber/?text=urlencodedtext ambapo whatsappphonenumber ni namba ya simu iliyo kwenye muundo kamilifu wa kimataifa urlencodedtext ni URL ya ujumbe usimbaji uliojazwa mapema.
Kwa mfano: https://wa.me/1XXXXXXXXXX?text=I'm%20interested%20in%20your%20car%20for%20sale
Kuunda kiungo kilichojazwa mapema na ujumbe, tumia https://wa.me/?text=urlencodedtext
Mfano: https://wa.me/?text=I'm%20inquiring%20about%20the%20apartment%20listing`
Baada ya kubofya kiungo, utaonyeshwa orodha ya waasiliani unaoweza kuwatumia ujumbe.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La