Ninawezaje kubadili mlio wangu kwa ajili ya WhatsApp?

iPhone
Kwenye iPhone, hakuna njia ya kuchagua mlio wowote isipokuwa ule unaopatikana ndani ya WhatsApp. Unaweza kubadilisha mlio wa simu wakati programu imefungwa kupitia Mipangilio ya WhatsApp > Arifa. Hapa unaweza kuchagua milio tofauti kwa ujumbe, ujumbe wa kikundi na Simu za WhatsApp.
Kwenye iOS 12 na miunganisho ya simu za wahusika wengine, mlio unaotumiwa kwa simu za sauti za WhatsApp ni mlio uliowekwa kwenye maelezo ya mawasiliano ndani ya programu ya Anwani kwenye simu.
Ili kuweka mlio maalum kwa simu za sauti za WhatsApp kwenye iOS 12:
  1. Nenda kwenye programu yako ya Anwani katika iPhone.
  2. Gusa mtumiaji unayetaka kumchagulia mlio maalum.
  3. Gusa Hariri katika kona ya juu kulia kwenye skrini.
  4. Chagua mlio wa simu.
  5. Anzisha iPhone yako upya.
Kumbuka:
  • Sauti maalum za arifa za ujumbe zinaweza kuwekwa katika Mipangilio ya WhatsApp > Arifa.
  • Simu za kikundi hutumia mlio chaguomsingi wa simu. Mlio huo wa simu hauwezi kugeuzwa unavyopendelea.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La