Maelezo ya jalada la mwenye anwani hayaonekani

Mipangilio ya faragha inakuruhusu kuficha mara yako ya mwisho kuonwa, picha ya jalada, taarifa kukuhusu, hali au taarifa za kusomwa. Huenda usione maelezo ya mtu mwingine kwa sababu ya jinsi alivyoweka mipangilio yake ya faragha.
Ikiwa huoni mara ya mwisho ya mtu kuonwa, picha ya jalada, taarifa kumhusu, hali au taarifa za kusomwa, inaweza kuwa ni kwa sababu ya moja ya yafuatayo:
  • Kuna hitilafu ya mtandao kwa muda mfupi.
  • Wewe au mtumiaji huyo mwingine mmebadili mipangilio ya faragha ya mwisho kuonwa au picha ya jalada.
  • Wewe na mtumiaji mwenzako mnahitaji kusawazisha anwani zenu.
  • Mtumiaji huyo amekuzuia.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La