Jinsi ya kuweka au kutoa soga au kikundi nyarakani

Kipengele cha kunyarakisha soga kinakuruhusu kuficha soga za binafsi au za kikundi kutoka kwenye orodha yako ya SOGA ili kupangilia mazungumzo yako vizuri.
Kumbuka:
 • Kunyarakisha soga hakufuti soga au kuhifadhi nakala ya soga kwenye iCloud.
 • Soga binafsi au za kikundi zilizonyarakishwa zitabakia nyarakani utakapopokea ujumbe mpya kutoka kwa mtu huyo au soga ya kikundi.
 • Unaweza kuona ni soga ngapi za binafsi au za kikundi zilizo na ujumbe mpya kwa kutelezesha hadi juu ya skrini ya SOGA.
Kunyarakisha soga au kikundi
 1. Katika kichupo cha Soga, telezesha kushoto kwenye soga au kikundi unachotaka kunyarakisha.
 2. Gusa Nyarakisha.
Unaweza kunyarakisha soga zote mara moja kwa kwenda kwenye Mipangilio ya WhatsApp > Soga > Nyarakisha Soga zote.
Kuona soga au vikundi vilivyonyarakishwa
 1. Telezesha hadi juu ya kichupo cha Soga.
 2. Gusa Soga Zilizonyarakishwa.
Kutoa soga au kikundi nyarakani
 1. Kwenye skrini ya Soga Zilizonyarakishwa, telezesha kushoto kwenye soga au kikundi unachotaka kukitoa nyarakani.
 2. Gusa Toa nyarakani.
Unaweza kuondoa soga nyarakani wewe mwenyewe kwa kutafuta jina la mwasiliani au ujumbe kutoka kwa mwasiliani huyo:
 1. Kwenye kichupo cha Soga, gusa upau wa Tafuta.
 2. Weka jina la soga au maudhui kutoka kwenye soga unayotaka kuitoa nyarakani.
 3. Telezesha kushoto kwenye soga unayotaka kuitoa nyarakani.
 4. Gusa Toa nyarakani.
Mipangilio mbadala ya kunyarakisha
Kubadilisha mipangilio chaguomsingi ili soga zilizonyarakishwa zitoke nyarakani ujumbe mpya unapopokelewa:
 1. Fungua Mipangilio ya WhatsApp.
 2. Gusa Soga.
 3. Zima Soga zibakie nyarakani.
Rasilimali zinazohusiana:
Jinsi ya kunyarakisha au kutoa nyarakani soga au kikundi: Android | Web na Desktop | KaiOS
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La