Kuhusu kuunda jina la biashara

Jina la biashara ni lazima iwakilishe biashara au shirika.
Sheria za kuunda jina la biashara
Ili kustahili kupata “Akaunti rasmi ya biashara", majina ya biashara hayawezi kuwa na:
 • Herufi zote kubwa, ispokuwa vifupisho. Herufi ya kwanza tu ndiyo inaweza kuwa kubwa, viunganisho haviwezi kuwa kwa herufi kubwa. Kwa mfano:
  • Sahihi: Vitafunio Vitamu au Burrito za Tammy na Tako
  • Sio Sahihi: VITAFUNIO VITAMU* au Burrito za Tammy Na Tako
 • Nafasi yoyote ya ziada kati ya maneno. Majina ya biashara lazima yatumie nafasi moja.
 • Uwekaji wa vituo vya uandishi usiohitajika
 • Emoji
 • Ishara (mfano: ®)
 • Mfululizo wa vibambo visivyo vya alfabeti na nambari (vibambo ambavyo ni vya nambari wala herufi)
 • Zozote kati ya vibambo hivi vya maalum: ~!@#$%^&*()_+:;"'{}[]\|<>,/?
Dondoo: Miongozo hii ya uumbizaji haitumiki kwa biashara ambazo tayari chapa zao ziko hivyo kwa nje. Katika kesi hiyo, jina la biashara linalotumika kwenye WhatsApp Business linaweza kuingiza uakifishi, herufi kubwa, nk kwamba inalingana na chapa ya nje.
Pia, majina ya biashara hayawezi kuwa na:
 • Jina kamili la mtu
 • Neno la kawaida (mfano: Mtindo)
 • Eneo la kawaida la kijiografia (mfano: New York)
 • Chini ya vibambo vitatu
Hatimaye, majina ya biashara hayawezi kuwa na mfano wowote wa neno "WhatsApp". Jifunze zaidi kwa kutembelea Miongozo ya Chapa/Bidhaa.
Dondoo: Ikiwa akaunti yako ya biashara imeorodheshwa kama "Akaunti rasmi ya biashara", kubadilisha jina lako la biashara kunaweza kusababisha akaunti yako kupoteza hadhi yake ya "Akaunti rasmi ya biashara".
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La