Jinsi ya kusambaza ujumbe

Tumia kipengele cha kusambaza ili usambaze ujumbe kutoka kwenye soga ya binafsi au ya kikundi kwenda kwenye soga nyingine ya binafsi au ya kikundi. Ujumbe uliosambazwa huashiriwa kwa lebo “Ulisambazwa” ili kukusaidia kujua kama rafiki au ndugu yako aliandika ujumbe aliotuma au ikiwa ujumbe huo ulitoka kwa mtu mwingine hapo awali.
Unaposambaza ujumbe, unaweza kuushiriki kwenye hadi soga tano kwa wakati mmoja. Ikiwa ujumbe tayari umesambazwa, unaweza kuusambaza kwenye hadi soga tano, ikiwa ni pamoja na kwenye soga moja ya kikundi. Ujumbe ukiwa umesambazwa mara nyingi, unaweza tu kusambazwa kwenda kwenye soga moja kwa wakati.

Kusambaza ujumbe
  1. Kwenye soga ya binafsi au ya kikundi, gusa na ushikilie ujumbe unaotaka kuusambaza, kisha gusa Sambaza.
    • Kusambaza ujumbe kadhaa, unaweza kuchagua ujumbe zaidi baada ya kuchagua ujumbe wa kwanza.
  2. Gusa Sambaza
    .
  3. Tafuta au chagua soga za binafsi au za kikundi unazotaka kuzisambazia ujumbe.
  4. Gusa Sambaza.
Kumbuka:
  • Unaweza pia kusambaza maudhui, mahali au anwani ili usiwe na ulazima wa kuzipakia tena.
  • Ujumbe wowote unaousambaza ambao si ujumbe wako unaotuma utakuwa na maneno “Ulisambazwa” kwako na kwa kila mpokeaji anayepata ujumbe huo.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La