Jinsi ya kuzuia usambazaji wa taarifa potofu

Fahamu kuhusu alama za ujumbe uliosambazwa
Ujumbe ukiwa na lebo ya “ulisambazwa”, hukusaidia kubaini kama ndugu au rafiki yako aliandika ujumbe au ikiwa ulitoka kwa mtu mwingine. Ujumbe ukisambazwa kupitia soga tano au zaidi, ikiwa ina maana kwamba umesambazwa angalau mara tano tangu mtumaji wa kwanza, aikoni ya vishale viwili
na lebo ya “Umesambazwa mara nyingi” itaonekana. Ikiwa huna uhakika ni nani aliyeandika ujumbe halisi, hakikisha ni ukweli. Kupata maelezo kuhusu kikomo cha kusambaza, rejelea makala haya.
Kuwa makini na unavyoamini
Jihadhari na taarifa ambazo zinathibitisha mambo ambayo tayari unayaamini; chunguza ukweli mwenyewe kabla ya kushiriki taarifa. Hadithi ambazo zinaonekana kuwa vigumu kuamini mara nyingi huwa si za kweli.
Chunguza taarifa kwa vyanzo vingine
Mara nyingi habari ghushi huenea sana, picha, sauti zilizo rekodiwa na video zinaweza kuhaririwa ili kukupotosha. Hata kama ujumbe umeshirikiwa mara nyingi, hilo haliufanyi kuwa wa kweli. Ukipokea taarifa ambayo ni ghushi, mjulishe mtumaji aliyekutumia taarifa ambayo si sahihi na umpendekezee kwamba awe akithibitisha ujumbe kabla ya kushiriki.
Ikiwa huna uhakika kama ujumbe ni wa kweli, tunapendekeza uangalie tovuti za kuaminika za habari kuona ni wapi habari hizo zilitoka. Habari ikiripotiwa katika maeneo mengi na kutoka kwenye vyanzo vinanvyoaminika, inawezekana kabisa kuwa kweli. Unaweza kuwasiliana na wakaguzi wa ukweli au watu unaowaamini, kwa taarifa zaidi. Kwa orodha ya wakaguzi wa ukweli walio na ushirika na Mtandao wa Kimataifa wa Ukaguzi wa Ukweli, angalia makala haya.
Ikiwa mwasiliani anatuma taarifa ghushi kila wakati, mripoti. Ili upate maelezo kuhusu jinsi ya kuripoti ujumbe, mwasiliani au kikundi, soma makala haya.
Kuwa makini na ujumbe ambao unaonekana kuwa tofauti
Ujumbe na viungo vingi visivyohitajika ambavyo unaweza kupokea huwa makosa ya tahajia au sarufi au hukuuliza ushiriki taarifa binafsi. Ili upate maelezo kuhusu jinsi ya kutambua na kushughulikia aina hizi za ujumbe, soma makala haya.
Kumbuka: Ikiwa unajisikia kuwa wewe au mtu mwingine yuko katika hatari ya kihisia au kimwili, tafadhali wasiliana na mamlaka ya kutekeleza sheria mahali ulipo. Mamlaka ya kutekeleza sheria yana vifaa vya kusaidia katika mambo haya.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La