Jinsi ya kuunda na kudumisha katalogi

Wavuti na Kompyuta ya dawati
Android
iPhone
Katalogi iliyosasishwa huwarahisishia wateja kutangamana na biashara yako. Pia, husaidia kuonyesha bidhaa na huduma zako mpya.
Kuweka bidhaa au huduma
Ili uweke bidhaa au huduma kwenye katalogi yako:
 1. Fungua programu ya WhatsApp Business.
 2. Bofya Zaidi
  |
  juu ya orodha yako ya soga > Katalogi.
 3. Bofya Ongeza bidhaa mpya.
 4. Bofya Ongeza Picha ili upakie picha kutoka kwenye faili zako. Unaweza kupakia hadi picha 10.
 5. Weka jina la bidhaa au huduma. Unaweza pia kuweka taarifa za hiari kama vile bei, maelezo, kiungo na msimbo wa bidhaa unayopakia.
 6. Gusa ONGEZA KWENYE KATALOGI ili uweke bidhaa kwenye katalogi yako.
Kumbuka: Kuweka bei kwenye katalogi kunapatikana katika baadhi ya nchi pekee.
Kudhibiti bidhaa au huduma ambazo wateja wanaweza kuona
Kumbuka: Huenda bado usiweze kutumia kipengele hiki.
Kuficha bidhaa za katalogi
 1. Fungua programu ya WhatsApp Business.
 2. Bofya Zaidi
  |
  juu ya orodha yako ya soga > Katalogi.
 3. Bofya bidhaa au huduma unayotaka kuificha > Hariri.
 4. Chagua Ficha bidhaa.
 5. Bofya Hifadhi.
Au, fanya kiashiria cha kipanya chako kielee juu ya bidhaa kwenye skrini ya Katalogi. Kisha, bofya Zaidi
|
> Ficha bidhaa.
Bidhaa zilizofichwa bado zitaonekana kwenye kidhibiti chako cha katalogi zikiwa na
kwenye picha ya bidhaa. Ukifungua ukurasa wa maelezo ya bidhaa, utaona pia dondoo inayoonyesha kuwa umeficha bidhaa hii.
Kufichua bidhaa za katalogi
 1. Fungua programu ya WhatsApp Business.
 2. Bofya Zaidi
  |
  juu ya orodha yako ya soga > Katalogi.
 3. Bofya bidhaa au huduma unayotaka kuifichua > Hariri.
 4. Ondoa uteuzi Ficha bidhaa.
 5. Bofya Hifadhi.
Au, fanya kiashiria cha kipanya chako kielee juu ya bidhaa kwenye skrini ya Katalogi. Kisha, bofya Zaidi
|
> Onyesha bidhaa.
Kufuta bidhaa au huduma
Ili ufute bidhaa au huduma kutoka kwenye katalogi yako:
 1. Fungua programu ya WhatsApp Business.
 2. Bofya Zaidi
  |
  juu ya orodha yako ya soga > Katalogi.
 3. Chagua bidhaa au huduma ambayo ungependa kufuta.
 4. Sogeza hadi chini kwenye sehemu ya maelezo ya bidhaa.
 5. Bofya Futa Bidhaa.
 6. Bofya SAWA.
Kumbuka: Kila picha inayopakiwa kwenye katalogi itakaguliwa. Ukaguzi husaidia kuthibitisha kuwa picha, bidhaa au huduma zinatii Sera za Biashara kwenye WhatsApp.
Ikiwa bidhaa au huduma katika katalogi yako imekataliwa, aikoni nyekundu ya mshangao itaonyeshwa karibu na picha. Ikiwa unahisi hii si sawa na ungependa kuomba ukaguzi mwingine:
 • Chagua bidhaa au huduma iliyokataliwa ili uone Maelezo.
 • Bofya omba ukaguzi mwingine.
 • Weka sababu ya ombi katika sehemu ya matini.
 • Bofya Endelea.
Kumbuka:
Ikiwa akaunti yako ya WhatsApp Business imeunganishwa na duka la Facebook na umeruhusu WhatsApp kuwa kituo cha mauzo, nafasi ya katalogi yako ya WhatsApp itachukuliwa na duka lako la Facebook kwa chaguomsingi. Hatua hii haitafuta au kubadilisha katalogi yako ya WhatsApp, lakini wewe na wateja wako hamtaiona. Unaweza kurudi kwenye katalogi yako ya WhatsApp wakati wowote kwa kuzima au kuficha WhatsApp isiwe kituo cha mauzo. Pata maelezo ya jinsi ya kudhibiti kituo chako cha mauzo kwenye Kidhibiti cha Biashara katika makala haya.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La