Â
Kuhusu "mwisho kaonwa" na "mtandaoni"
Mwisho kaonwa na mtandaoni hukuambia muda wa mwisho ambapo watu unaowasiliana nao walitumia WhatsApp, au ikiwa wapo mtandaoni.
Ukiona mtu unayewasiliana naye yupo mtandaoni, basi amefungua WhatsApp kwenye kifaa chake na ameunganishwa kwenye intaneti. Hata hivyo, haimaanishi kuwa mtumiaji amesoma ujumbe wako.
Kipengele cha mara ya mwisho kuonwa hurejelea muda ambao mtu unayewasiliana naye alitumia WhatsApp mara ya mwisho. Kupitia mipangilio yetu ya faragha, una chaguo la kudhibiti nani anaweza kuona mara ya ulipoonekana na ulipokuwa mtandaoni. Huenda usiweze kuona maelezo ya mtu kuhusu mara ya mwisho kuonwa au kuwa mtandaoni isipokuwa kama amekuhifadhi katika anwani zake au alikutumia ujumbe hapo awali.
Unaweza kutumia mipangilio ili udhibiti nani anaweza kuona maelezo yako ya mara ya mwisho kuonwa au kuwa mtandaoni. Fahamu namna ya kufanya hivyo.
Kuna sababu kadhaa zinazoweza kufanya usione mara ya mwisho kuonwa au kuwa mtandaoni kwa mtu mwingine:
- Anaweza kuwa ameweka mipangilio yake ya faragha ili kuficha maelezo haya.
- Huenda umeweka mipangilio yako ya faragha ili usishiriki maelezo yako ya mara ya mwisho kuonwa. Ikiwa hushirikishi mwisho wa kuonwa kwako, hutaweza kuona mwisho wa kuonwa kwa watu wengine unaowasiliana nao.
- Unaweza kuwa umezuiliwa.
- Huenda hujapiga soga naye hapo awali.
- Huenda hajahifadhi namba yako kwenye anwani zake.
- Huenda hujahifadhi namba yako kwenye anwani zako.
Kumbuka: Watu waliopo mtandaoni kwenye mazungumzo ya soga na wewe wanaweza kuona unapoandika.
Rasilimali zinazohusiana: