Mahitaji ya kutangaza ujumbe

Kipengele cha Orodha ya Tangazo kinakuruhusu kutuma ujumbe au media kwa waasiliani kadhaa kwa mara moja. Ujumbe wa tangazo utaonekana kuwa ujumbe wa kibinafsi kutoka kwako.
Mahitaji ya tangazo la ujumbe:
  • Hakikisha kuwa anwani zote katika orodha ya tangazo zimehifadhi namba yako katika vitabu vyao vya anwani.
  • Hakuna kikomo kwa idadi ya orodha ya tangazo unazoweza kuunda.
  • Unaweza kuchagua hadi waasiliani 256 kwa kila Orodha ya tangazo.
Ili kuhakikisha kuwa jumbe zinatolewa kwa usahihi, tunashauri usitangaze jumbe nyingi kwa wakati mmoja.
Jifunze zaidi kuhusu kutumia Orodha ya Tangazo kwenye: Android | iPhone
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La