Kuhusu nakala za soga kwenye Hifadhi ya Google

Android
Njia rahisi zaidi ya kuhamishia data yako ya WhatsApp kwenye simu mpya ni kwa kutumia Hifadhi ya Google. Hifadhi ya Google inatolewa, inatengenezwa na kuendeshwa na Google. Tunapendekeza uunganishe simu yako kwenye Wi-Fi kabla ya kuhifadhi nakala ya soga zako katika Hifadhi ya Google, kwa sababu faili za nakala rudufu zinaweza kuwa za ukubwa tofauti, hivyo kutumia data ya simu na kukusababishia gharama za ziada. Kuanzia tarehe 19 Aprili, 2022, utahitaji kuhifadhi nakala kwenye Hifadhi ya Google kila baada ya miezi 5 ili uepuke hasara ya kufutiwa.
Kumbuka:
  • Nakala rudufu za WhatsApp hazihesabiwi katika mgawo wa nafasi ulio nao kwenye Hifadhi ya Google.
  • Nakala rudufu za WhatsApp zinahusiana na namba ya simu na akaunti ya Google ambazo ziliundwa.
  • Nakala rudufu za WhatsApp ambazo hazijasasishwa baada ya miezi 5 zinaweza kuondolewa kiotomatiki na Google. Ili usipoteze nakala zozote rudufu, tunapendekeza uhifadhi nakala yako ya data ya WhatsApp mara kwa mara.
  • Nakala rudufu ya kwanza inaweza kuchukua muda kukamilika. Tunapendekeza uache simu yako ikiwa imeunganishwa kwenye chanzo cha umeme.
  • Kila wakati unapotengeneza nakala rudufu kwenye Hifadhi ya Google kwa kutumia akaunti ile ile ya Google, nakala rudufu ya awali itabadilishwa na Google. Hakuna njia ya kurejesha nakala rudufu ya zamani ya Hifadhi ya Google.
  • Maudhui na ujumbe unaohifadhi haulindwi kwa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho wa WhatsApp ukiwa kwenye Hifadhi ya Google isipokuwa ukichagua kuwasha ufumbaji wa nakala rudufu mwisho hadi mwisho.
Tafadhali rejelea makala haya ya kituo cha msaada mara kwa mara ili upate habari mpya.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La